Kocha maarufu kwa jina la Super Coach Sylversaid Mziray 'Mwanangu' amefariki dunia jana asubuhi katika hospitali ya AgaKhan jijini Dar es salaam alikokuwa amelazwa kwasiku kadhaa zilizopita.
atakumbukwa na wapenzi wa soka kwa mchango wake mkubwa wa mawazo na wa kivitendo . Amewahi kuzifundisha timu za simba na Yanga pamoja na Taifa Stras kwa nyakati tofauti. Tunamuomba Mwenyezi Mungu Aiweke roho ya Mziray peponi , Amin...
Marehemu Syllersaid Mziray, enzi za uhai wake.
Taarifa ya MAKAMU Mkuu WA Chuo Kikuu Huria cha Tanzania, Profesa Tolly S.A. Mbwette, kwa niaba ya Menejimenti yote ya Chuo,imetoa tamko juu ya msiba huo wa mkufunzi wake wa michezo, Syllersaid Mziray.
"Mziray alifariki dunia alfajiri ya kuamkia leo Jumamosi katika hospitali ya Aga Khan alikokuwa amelazwa kwa karibu wiki mbili kutokana na Malaria na baadaye matatizo ya figo.Taratibu za Mazishi zinaendelea nyumbani kwake Tabata Magengeni. Mziray atazikwa Jumatatu kwenye Makaburi ya Kinondoni.
Mazishi hayo yatatanguliwa na utoaji wa heshima hapa chuoni.Mungu ailaze roho ya marehemu Syllersaid Mziray Pema Peponi Amen!", taarifa hiyo ilimaliziwa na kusainiwa na KURUGENZI YA MAWASILIANO NA MASOKO kwa niaba ya Chuo hicho
Ni hapa...
Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!
Posted by
BM.
on
Sunday, October 31, 2010
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment