Ni hapa...

Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!

Posted by BM. on Tuesday, April 12, 2011

Aliyekuwa rais wa Ivory Coast, Laurent Gbagbo ambaye alijiapisha mwenyewe kuwa rais baada ya kushindwa kwenye uchaguzi amekamatwa na wanajeshi wa mpinzani wake Allassane Ouattarra.
Inadaiwa na vyombo vya habari vya magharibi kuwa alilia akiomba asiuwawe baada ya kuingia kwenye mikono ya mpinzani wake.Kilikuwa kipindi kigumu kwake pale alipojikuta akivamiwa handakini akiwa yeye na mke wake na mwanawe wa kiume .


"Msiniue tafadhali", hilo ndilo lilikuwa neno la kwanza la rais Gbagbo baada ya kutiwa mikononi mwa majeshi ya mpinzani wake.Gbagbo alivalishwa jaketi lisilopitisha risasi ili kumlinda kutokana na wanajeshi wenye hasira ambao walitaka auliwe wakati huo huo bila ya kumchelewesha.Alipakizwa kwenye gari na kupelekwa kwenye makao makuu ya kambi ya Ouattara iliyopo kwenye hoteli ya Golf Hotel.


Ouattara akiongea kwenye televisheni ya taifa aliwataka wananchi wa Ivory Coast washikamane baada ya kutiwa mbaroni kwa mpinzani wake mkuu, Laurent Gbagbo.Ouattara alitamba kuwa nchi yake inaingia kwenye ngwe mpya ambapo aliahidi ataunda tume kuchunguza mauaji yaliyofanyika wakati wa vita hivyo vya wenyewe kwa wenyewe.
Inaelezwa kuwa mwanajeshi mmoja alimpiga kibao Gbagbo wakati wa kumkamata alipotoa majibu kana kwamba ni kiongozi wa nchi, jambo ambalo lilimuudhi mwanajeshi huyo ambaye alishajitoa muhanga hadi kumfikia hapo alipo.

0 comments: