Ni hapa...

Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!

Posted by BM. on Sunday, April 17, 2011

Pilika pilika za uchaguzi zinaendelea kote nchini Japani wakati huu kwa staili yake ambapo leo Jumapili chaguzi katika kanda maalum hapa zinazojulikana kama (dai-jūnana-ai tōitsu chihō senkyo)zinafanyika. Japani ni nchi ya vyama vingi vya siasa.

Uchaguzi mwingine ulifanyika jumapili iliyopita ambapo magavana 13 , mabaraza ya kimkoa na mameya watano pamoja na wajumbe kutoka mabaraza 16 walichaguliwa.La ziada ni kuwa kuna mabango maalum yenye nambari ambapo kila chama hulipia kisanduku chake nchi nzima kwa kila bango ambapo hubandika picha ya mgombea na madokezo muhimu. Kama hujisshughulishi huwezi kujua...kuko shwari tu. Pilika pilika hizi zitakamilika jumapili ijayo.
Pengine jipya ukilinganisha na nyumbani...kampeni za hapa ni za kisayansi. Mitandao ya wavuti imetumika sana, magari machache yamekuwa yakipita kuwakumbusha maeneo ya kupigia kura kwa wale wenye sifa hizo.

Wagombea wamekuwa wakijitokeza maeneo ya wazi kama vile vituo vya treni na kunadi sera zao lakini watu wachache tu husikiliza kwani taarifa wanazo kupitia wavuti. Picha za wagombea hubandikwa kwa utaratibu maalum, na hulipiwa kwa mammlaka zinazohusika.

Hata miye nimepokea vipeperushi wa wagombea , lakini sina haki ya kupiga kura naangalia tu basss!

0 comments: