Mwanamitindo, mtangazaji wa michezo ya kubahatisha na binti anayejipenda sana Bi.Kayo Sato (a.k.a Kayo Police)amewaacha watu vinywa wazi pale aliposema kuwa ana siri kubwa sana moyoni mwake inayohusu jinsia yake. Kufuatia maneno ya chini chini ya muda mrefu, binti huyo ambaye sasa ana miaka 23 alikwenda kwenye kituo kimoja cha Televisheni na kusema kuwa kwa hakika yeye ni mwanaume na si mwanamke ...ila anapenda kuwa katika muonekano wa kike.Kayo ni maarufu sana hapa Japani kwa kusimamia maonyesho yanayojulikana kama 'The Nico video game show.
Bi. Kayo anasema kuwa aliondoka kwenye mji wa kwao kipindi kidogo, na sio rahisi kwa watu waliokuwa wakimjua awali kujua kuwa ni mwanaume na akaanza kuishi kama mwanamke kwa kutumia majina mengine.
Alijiunga na shirika la wanamitindo na kujizolea umaarufu mkubwa kama mdada modeli wa kutumainiwa na katika kwa kipindi chote cha miaka kadhaa hakuna mtu katika shirika lake aliyewahi kumgutukia.
Anasema wala hajafanyiwa upasuaji wa ngozi na kuwekewa vipande bandia, yeye ana uzuri wa asili na amepata mafanikio makubwa katika kazi yake kwa kutumia vipodozi tu. Bi. Kayo aliandika katika blogi moja hapa Japani kuwa , "Kwa yeyote aliyepokea ujumbe wangu, asante sana kwa maoni yenu, nimetiwa moyo sana na maoni yenu, na kaa nilivyosema kwenye maonyesho yale mie nilizaliwa mvulana,niliona litakuwa jambo jema kumwambia kila mtu juu ya yale yanayonihusu , yaliyopita. Nimefarijika kwa kunipa fursa hii na , nitafanya kazi kama Kayo Sato na kuendelea mbele, na nina furaha sana kuwa watu wengi wamenikubali na kukubali mwanzo wangu huu mpya".
Tangu wakati alipoweka wazi jinsia yake kwemye blogi amekuwa akipokea ujumbe wa kumtia moyo kutoka kwa watu wengi. Source; webs za kijapani..
Ni hapa...
Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!
Posted by
BM.
on
Sunday, June 26, 2011
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment