Jioni ya leo Mie na mbongo mwenzangu Mr. Eustadius Francis (Anasoma Chuo Kikuu cha kilimo cha Tokyo)tulikwenda katika mgahawa wa Tsuraya eneo la Setagaya, mkabala na Chuo kikuu hicho kupata kikombe cha kahawa. Jambo lililotufurahisha sana ni kukutana na bidhaa ya tanzania ikinadiwa!
Kahawa ya Tanzania...pamoja na tangazo maalum kuelezea ubora wa bidhaa hiyo.
Kwahakika ilibidi tuinunue na kula kile cha nyumbani...tulifarijika sana. Tulitamani kusema kwa sauti kuwa 'hii kahawa inatoka kwetu! '..pengine siku nyingine! Hongereni wote waliofanikisha jambo hili...
Ni hapa...
Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!
Posted by
BM.
on
Saturday, June 18, 2011
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment