Ni hapa...

Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!

Posted by BM. on Saturday, June 18, 2011

Raisi wa zamani wa Zambia , Fredrick Chiluba amefariki dunia leo Jumamosi june 18 jijini Lusaka akiwa na miaka 68..Kwa mujibu wa Msemaji wake Emmanual Mwamba , Hadi jana ijumaa Bw. Chiluba alikuwa mzima wa afya akifanya mikutano yake ya kisiasa lakini baadaye jioni aliwaita madaktari wake akilalamika kuwa hakuwa anajisikia vyema na usiku wake akaaga dunia. Unaweza kujikumbusha safari yake ya maisha kwa njia ya video...
Chiluba aliingoza nchi hiyo kwa vipindi viwili baada ya kumshinda kwa kura mwasisi wa taifa hilo Raizi wa zamani Kenneth Kaunda aliyekaa madarakani kwa miaka 27. Siku za katikati alipata misukosuko mikubwa ya kisiasa ikiwa ni pamoja na kuelezwa kuwa ametumia sivyo ndivyo Dola laki tano za kimarekani mali ya Ikulu kinyume cha Sheria lakini hatimaye akaipangua kesi hiyo. Hata hivyo wake wake Regina Chiluba alikabiliwa na mashitaka na akashindwa mahakamani na kujikuta jela hata hivo alikataa rufaa na kuachiwa...
Habari: Magazeti ya Zambia..

0 comments: