Mwalimu wa Chuo cha Kilimo cha Mtwara Bw. Muhaji Abdallah Lenga (Pichani)yupo nchini Japani kuongeza ujuzi wa kilimo cha mpunga, kwasasa yupo eneo la Chiba. Idhaa ya Kiswahili ya Redio Japani ilibahatika kuongea naye. katika kipindi chote cha kuwa hapa Japani amekuwa akijibiidisha kwa nadharia na vitendo katika kujielimisha juu ya kilimo cha zao hilo. Moja ya mambo yaliyonifurahisha sana katika mazungumzo yetu ni matumizi ya bata wakula magugu katika mashamba ya mpunga hapa Japani. angalia Picha za mabata hao wakiwa kazini.
Mwl . Lenga amesema kuwa Bata hawa ni chotara , mchanganyiko wa bata maji na bata kama wale wa nyumbani kwahiyo wanauwezo wa kuishi majini wakiwekwa huumo tangu upandaji wa mpunga hadi kuvunwa na baadaye hutumika kama kitoweo. Bata hawa wanafundishika na hawawaogopi binaadamu. Lengo la kuwatumia mabata hawa ni kupalilia mashamba kwa kula magugu na kuongeza mbolea kwa kinyesi chao. Hii ni mbinu ya kitaaluma ya kukwepa kutumia madawa ya kuuwa wadudu au kemikali. Kemikali zina athari kubwa mashambani na kwa walaji. Kwa mujibu wa Mwl Muhaji, uzalishaji wa mpunga kwa kuwatumia mabata hawa ni wa gharama ya juu ,ikilinganishwa na ule wa matumizi ya madawa ya kuuwa wadudu ya viwandani. Wajapani wanazingatia sana kanuni za kilimo na ndi maana wanapata mavuno mengi katika ekari moja..
Ni hapa...
Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!
Posted by
BM.
on
Saturday, June 18, 2011
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment