Ni hapa...

Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!

Posted by BM. on Thursday, June 23, 2011

Jana Jumanne 21/06 kulikuwa na hafla maalum katika Chuo Kikuu cha Kilimo cha Tokyo hapa japani iliyowajumuisha wanafunzi kutoka mataifa mbalimbali duniani inayofahamika kama 'International Students Party' kwa kisukuma " (留学生 パーティー)" Party hii hufanyika kila mwaka ambapo wanafunzi kutoka nchi zisizopungua 19 wanaosoma Chuoni hapo husherekea pamoja na wenyeji wao. Ambatana nami...
Katika sherehe hizo vyakula vyenye asili ya Nchi tofauti huandaliwa na pia wanafunzi hutoa burudani mbalimbali ikiwa ni sehemu ya kubadilishana utamaduni. Kwa Mwaka huu, wanafunzi kutoka Tanzania waliandaa Ndizi Nyama zilizoungwa kwa tui zito la nazi viungo mbalimbali na mchuzi saafi wa maharage yaliyoungwa kwa nazi. Chakula hiki kiliwashangaza wengi. kwani kwa utamaduni wa Japan na nchi nyingi barani Asia hutumia ndizi kama tunda tu.
Maelezo yalitolewa na kila nchi kama alivyofanya mdau hapo Eustadius Francis kutoka Tanzania -Pichani...


Kwa upande wa burudani, vijana walishusha Sebene zito ambalo liliwafanya watu kutoka nchi mbalimbali kuja Kushambulia jukwaa. Hata hivyo mwisho wa party hiyo rasmi, ulikuwa ndio mwanzo wa ''after party'',
Chanzo cha habari hii hakikuwa tayari kudadavua yaliyojiri huko pengine baadaye ...
Take 5 mdau E.F

1 comments:

Nahabonyeyo said...

Sawasawa kijana,naona c haba.. Kaka hlo sebene... I wsh ningelikuona Live Ukshusha vitu,. Congrats sana...e Ukshusha vitu,. Congrats sana...