Mwanamke mmoja raia wa Brazil anayeaminika kuwa na umri mkubwa kuliko binaadamu yoyote duniani amefariki akiwa na miaka 114. Maria Gomes Valentim alifariki dunia pale ogani zake muhimu, (viungo tete vilivyo muhimu ) Kuacha kufanya kazi kwa mpigo, ikiwa ni siku chache tu hajaingia mwaka wake wa 115.Record za Guinness duniani zinathibitisha kuwa bibi huyo alizaliwa mwaka 1896 na mwezi uliopita tu alitangazwa kuwa nashikilia rekodi hiyo ya kuwa mtu mwenye umri mkubwa duniani. Siku chache kabla ya kifo chake alionekana kufurahia mlo wa Ki-Brazil unaoitwa, feijoada, and n a mapochopocho yenye sosi za pilipili.Kwa mujibu wa rekodi ya Guinness, Bi. Valentim amefariki akiwa na umri wa miaka 114 years na siku 347 days na sehemu kubwa ya maishayake alikuwa katika mji wa Carangola, uliopo mashariki mwa Brazil. Awali ilikuwa ikijulikana kuwa mtu aliyekuwa na umri mkubwa alikuwa Besse Cooper wa Georgia, nchini Marekani lakini mwezi Uliopita ilibainika kuwa Valentim alikuwa mkubwa kwa siku 48 kuliko alivyo Cooper.Bibi huyo ameacha wajukuu wanne, watukuu saba na wajukuu wa wajukuu zake watano.
Ni hapa...
Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment