Ni hapa...

Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!

Posted by BM. on Saturday, May 02, 2009

Mtoto wa miaka miwili ambaye alianza kuzungumza alipokuwa na umri wa miezi nitano na kuanza kutembea akiwa na miezi minane ameweka rekodi kwa kuwa mwanachama mdogo kuliko wote kuingizwa kwenye jumuiya ya watu wenye akili na upeo usio wa kawaida ya MENSA; Mtoto Elise Tan Roberts mwenye umri wa miaka miwili ambaye IQ yake imepishana kidogo na IQ ya mwanasayansi nguli wa fizikia Albert Einstein amekuwa ndio mwanachama mdogo kuliko wote kuingizwa kwenye jumuiya ya watu wenye akili sana zisizokuwa za kawaida inayoitwa MENSA.Ili kuwa mwanachama katika jumuiya ya MENSA inabidi mtu ufaulu kwa asilimia 98 au zaidi katika mtihani maalumu wa IQ.
Elise alianza kuzungumza alipokuwa na umri wa miezi mitano na kuanza kutembea alipofikisha miezi nane na hivi sasa akiwa na umri wa miaka miwili ana uwezo wa kutaja miji mikuu 35 duniani, kutaja na kuzipanga alphabet na kutaja majina yote ya maumbile ya pembe tatu."Huongea vitu ambavyo hukuacha mdomo wazi ukifikiria amevitoa wapi" alisema mama yake Louise mwenye umri wa miaka 28."Anapenda kujifunza vitu na huvishika katika muda mfupi".alisema mama yake. Mensa walithibitisha kwamba akiwa na umri wa siku 845 ( Miaka miwili na miezi minne) , Elise ndiye mwanachama mdogo kuliko wote wa Mensa, akimpiku Ben Woods, aliyeingizwa kwenye jumuiya ya Mensa alipokuwa na umri wa 1,035 mwaka 1990. IQ ya Elise ni 156 wakati mwanasayansi mkongwe wa fizikia Albert Einstein maarufu kwa kanuni yake ya nishati ya E = mc2 alikuwa na IQ ya 160.

0 comments: