Mahakama ya mji wa Munich nchini Ujerumani imemkuta na hatia ya kuamuru kufanyika kwa mauaji ya raia katika kijiji kimoja nchini Italia wakati wa vita vikuu vya pili vya dunia, kamanda wa zamani wa jeshi la WANAZI mwenye umri wa miaka 90 Josef Scheungraber na kumuhukumu kifungo cha maisha.Adhabu hiyo inafuatia kukutikana kwake na hatia ya makosa kumi ya mauaji pamoja mengine ya kujaribu kuua.Scheungraber alikuwa na cheo cha luteni na umri wa miaka 25 wakati mauaji hayo yalipofanyika karibu na mji wa Arezzo mwaka 1944 ambapo raia 14 waliuawa.Mauaji hayo inasemekana yalikuwa ni kulipiza kisasi kutokana na kuuawa wanajeshi wawili wa Ujerumani na wanaharakati wa Kitaliani.Tayari mtuhumiwa huyo alishahukumiwa na mahakama ya Italia kifungo cha maisha jela akiwa mwenyewe hayuko mahakamani.
Ni hapa...
Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!
Posted by
BM.
on
Friday, August 14, 2009
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment