Ni hapa...
Mkurugenzi wa filamu, Jason Russell, ambaye filamu yake inayomshambulia kiongozi wa wapiganaji wa Uganda, Joseph Kony, ilizagaa kwenye mtandao wa internet, inaelekea amepata ugonjwa wa akili.
Shirika lilofanya filamu hiyo, liitwalo "Invisible Children", limesema kuwa Bwana Russell amelazwa hospitali kutokana na machofu, kiwiliwili kuwa kikavu, na njaa.
Shirika la "Invisible Children", lilisema zogo lilozuka baada ya filamu hiyo, limesumbua roho za wanachama wote; na hasa Bwana Russell.Ripoti zinasema kuwa Jason Russell amekutikana hakujistri sawasawa, akipiga kelele mabara-barani, mjini San Diego, California.Filamu hiyo ya nusu saa, iliyotoa wito kuwa Joseph Kony akamatwe, ilizagaa kwenye mitandao, na kuwasikitisha wengi, lakini baadhi ya watu wanaona filamu haikueleza vita vya Uganda vilivyo.(BBC na Mitandao mingine)
Ni wimbo mzuri kwa wanaopenda muziki wa taratibu....
Tumetembelewa na Comrade mwenzetu kutoka Kenya , Muriithi Mutiga(Kushoto), huyu ni mwandishi wa habari wa Gazeti la The Nation - huko Kenya. Kushoto kwake ni Bi. Haruka Nakamura Fundi Mitambo katika Idhaa ya Kiswahili ya Redio Japani-NHK World ,Kushoto kwake ni mtangazaji Edward Kadilo anayetokea KBC -Kenya na kushoto kabisa mie BM...
Sikiliza tajiriba hii muhimu!....
Jiji la Tokyo lina eneo dogo sana kama ilivyo kwa nchi yenyewe ya Japani ikilinganishwa na eneo kama la Tazania. Lakini kilichofanikiwa kwa kiasi kikubwa ni matumizi mazuri ya eneo lake, miundombinu, na mazingira ya kiteknolojia.
Kilichonifurahisha mie zaidi ni kuwepo kwa misitu kadhaa katikati ya jiji hilo nammoja wapo ni huu uliopo karibu na jengo la Makao Makuu ya shirika la utangazaji la Japani NHK World -NHK World maarufu "Yoyogi Park". Nawaza hili mbona linashindikikana kwenye miji na majiji yetu kule nyumbani Tanzania. Msitu wa Kibaha ingewezekana ...lakini vibaka wameweka makazi kiasi cha wakazi wa eneo hilo wanataka msitu ufyekwe...du...tujifunze kutoka hapa basss..! Nawaza 2 !...
Hapo ndipo tulipofika sasa!...
Hapo ndipo tulipofika sasa!...
Fuatilia taarifa hii inajieleza yenyewe....