Ni hapa...
NIMEREJEA..... Wapenzi wa ukurasa huu wa MIRINDIMO, nawaomba radhi sana kwa kutokuweka kitu kipya kwa muda mrefu. Nilikuwa na dharura. Mtandao ulipata kwikwi iliyokaa mahala pabaya. Nimesaidiwa mpaka nimekwamuka. Namshukuru sana da Subi kule Marekani kwa ushauri wake wa kiufundi na Bro. Malkiory kule Finland. Tulikuwa nao kimyax2 wakinisaidia. bado niko katika hatua za mwisho za kuirejesha vilivyo ilivyokuwa. Nawashukuru mashabiki wote wa MIRINDIMO kwa uvumilivu. Msulwa.
Huyu mama ni mwanademokrasia wa Mynmar ...nafurahia snaavyojbu maswali...
Mkurugenzi wa filamu, Jason Russell, ambaye filamu yake inayomshambulia kiongozi wa wapiganaji wa Uganda, Joseph Kony, ilizagaa kwenye mtandao wa internet, inaelekea amepata ugonjwa wa akili.
Shirika lilofanya filamu hiyo, liitwalo "Invisible Children", limesema kuwa Bwana Russell amelazwa hospitali kutokana na machofu, kiwiliwili kuwa kikavu, na njaa. 
Shirika la "Invisible Children", lilisema zogo lilozuka baada ya filamu hiyo, limesumbua roho za wanachama wote; na hasa Bwana Russell.Ripoti zinasema kuwa Jason Russell amekutikana hakujistri sawasawa, akipiga kelele mabara-barani, mjini San Diego, California.Filamu hiyo ya nusu saa, iliyotoa wito kuwa Joseph Kony akamatwe, ilizagaa kwenye mitandao, na kuwasikitisha wengi, lakini baadhi ya watu wanaona filamu haikueleza vita vya Uganda vilivyo.(BBC na Mitandao mingine)
Ni wimbo mzuri kwa wanaopenda muziki wa taratibu....



