Ni hapa...

Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!

Posted by BM. on Sunday, February 28, 2010


Ni msichana anayejulikana kwa jina la Judith Omondi ambaye anakaridiwa kuwa na umri wa miaka 30. Judith ameshawahi kufanya kazi kama erotic dancer katika ya miji Tampere, Jyväskylä and Lahti nchini Finland . Maajabu ni kwamba Judith pamoja na kuwa alikuwa akijua wazi kuwa ni ameathirika na virusi vya ukimwi lakini ameendeleza tabia ya kutembea na wanaume wengi katika maeneo hayo na hadi sasa wanaume saba kati ya hao wameshatambulika. Kwa sasa Judith anashilikiliwa na polisi wa huko Finland. Bila shaka hii SI habari njema! Picha na habari kutoka mtandao wa Malkiory wa Tampere.

Posted by BM. on Sunday, February 28, 2010

Jana Jumamosi nilitembelewa na watu muhimu sana katika makazi yangu hapa Tokyo. Ilikuwa siku nzuri na nilifaidika sana na mada zilizoongelewa nyingi zikiwa za changamoto ya kimaisha. Mmoja wao alikuwa Mwenyekiti wa Jumuia ya watanzania waishio nchini Japani TANZANITE Dr. Ally Simba. Baada ya mazungumzo kilichofuata ni kupata rizki.

Komrade Amani (Kulia) na Francis Mosongo , Afisa wa Ubalozi wa Tanzania hapa Japani (Kushoto) walikuwepo katika mazungumzo haya ya kirafiki.

Nilihemewa kwa furaha kuwa na watu muhimu na kunimegea busara zao.

Mwenyekiti, Dr. Simba na mdau Reginald Ndesika , wakipata kitu kidogo huku mijadala ikiendelea.

Posted by BM. on Sunday, February 28, 2010


zoezi la kuwahesabu watoto na kuwapeleka shule linafanywa hivi sasa na shirika la Elimu , Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa -UNICEF huko Haiti.Maisha yanaanza upya baada ya kizazaa cha tetemeko.

Posted by BM. on Sunday, February 28, 2010

Jamaa mmoja huko Mansewhra nchini Pakistan alikwenda kwenye kituo kikuu cha Polisi kwa lengo la kukilipua kwa mabomu aliyojifunga nayo mwilini. Polisi walimgutukia walichofanya ni kumpiga risasi na kumuua palepale. Sasa ishu ilikuwa kuyaondoa mabomu vinginevyo jengo litalipuka. Kachero mmoja akajitosa na hapo anafanya kazi hiyo kwa tahadhali kubwa.

Posted by BM. on Thursday, February 25, 2010

Wanaomjua Mwanamuziki Dekula Kahanga ambaye sasa yuko Uarabuni wataguswa na habari hii ; kuwa amefyatua kibao kipya ...GOD is ONE. Unaweza kubofya hapo chini na kuanza kusikiliza kisha kujizungusha ruhsa.



Haya unasemaje...

Posted by BM. on Wednesday, February 24, 2010

Mdada Diva Meje naye amejitosa katika burudani ya muziki huko DRC anamtumia Tshala mwana kumuingiza uwanjani. Hebu sikiliza toleo lake hili na sauti ya Tshala mwana ikihanikiza.

Posted by BM. on Wednesday, February 24, 2010


Taarifa na burudani

Posted by BM. on Tuesday, February 23, 2010

Hivi sasa kuna Operesheni kali huko Afghanistan kuwasaka Wa-TALIBAN, Operesheni inayofanywa na majeshi ya NATO wakiongozwa na MAREKANI. Tuiangalie kwa njia ya picha.
Mzee huyo anayeongea anaitwa Haji Abdul mlimaji wa Afyuni -Opium kilevi kinachowapatia fedha nyingi wataliban ; hapa anahojiwa shambani kwake huko Qalanderrabad . Wanajeshi wa Marekani wameahidi kumlipa fidia kwa kuharibu mazao yake walipoteremka kwa parachuti hapo lakini kwa sharti awaambie walipo wa-Taliban. Sijui walimalizana vipi...

Mji umeteketezwa kabisa , kisibaki kitu...du aliyekuwemo na asiyekuwemo .Balaa. Eneo la Gandalobog, Afghanistani panapoaminika kuwa na makao makuu ya Wataliban. Vita si mchezo unakataa! eneo ambalo Majeshi ya Marekani wanaamini kuwa maroketi ya Taliban yanatokea. Sgt Darin Hendricks amepewa jukumu la kuiiangia ndani na kuchungulia ili kujua kukoje. kazi ipo!
Mwili wa mtu anayeshukiwa kuwa ni askari wa kundi la Taliban .Picha zote kwa hisani ya mtandao wa boston.

Posted by BM. on Monday, February 22, 2010


Maeneo mengi ya Japani kuna maeneo kama haya matakatifu kwa imani za kibudda kando ya barabara ama mitaani na watu hufika hapo kuendesha ibada fupix2 . Picha zaidi baadaye!

Posted by BM. on Monday, February 22, 2010


Shule ya kulelea watoto iliyo karibu na Jengo la Utangazaji , NHK hapa Tokyo . Kilichonifurahisha matunda kuivia mtini bila kupopolewa. Hii inakuwaje!

Posted by BM. on Monday, February 22, 2010

Leo nilitembelea mgahawa wa Kihindi eneo la Shibuya jijini Tokyo , chakula nilichochagua kilikuwa na pilipili kali na nilikimaliza chote ...pamoja na kibaridi kikali , kijasho kilinitoka. Hapo shughuli ilikwisha..
Shibe ya Chakula cha kihindi mwili unawaka kwa pilipili...

Posted by BM. on Saturday, February 20, 2010


Wakazi wa jiji la Kabul nchini Afghanistan hukusanyika nyakati za jioni kuona majogoo mawili yanavyoparurana kama ambavyo watu wa Japani wanavyoshabikia mchezo wa Mieleka wa Sumo. Timu inayotoka na ushindi kwa jogoo wake kumzidi mwenzake hufanya sherehe ya ushindi. kila mahali kuna mambo yake.

Posted by BM. on Saturday, February 20, 2010


Mwanasoka wa Kimataifa Diego Maradona akiwa ziarani Afrika Kusini alipowatembelea watoto wa shule moja ya sekondari na kupiga nao picha.

Posted by BM. on Saturday, February 20, 2010

Wadau wakijimwaya katika ukumbi wa Kiluvya Pub, Kibaha siku ya wapendao Feb 12. Aina ya muziki unaochezwa hapo, saaana ni Rhumba la kizamani. Nakuweke moja ya nyimbozinazotamba hao weekend. Bahati nzuri maandishi yana tafsiri ya kiingereza wacha nami niyatafsiri kwa kisukuma ,lugha ya kwetu.Soma kwanza tafsiri ya wimbo huo kwa kifupi halafu bofya usikilize wimbo wenyewe.
"Tumezungumza sana jana jioni,
lakini baadaye usiku usingizi uliruka kabisaa,
nilikuwa nikiuliza kama hili litaweza kuwa kweli?
Jambo ulilokuwa ukilizungumzia lilinishangaza kweli!"
"...Ninashangaa kwanini unanifanyia wivu, kwani tulikwishaachana na wewe umeoa kitambo,Huwa nakupokea mara kwa mara nyumbani nikidhani unakuja kumuona mtoto lakini cha kushangaza unaniambia eti tuwe wapenzi tena..Unajua !...siko peke yangu tena siku nyingi tu niko na Pedejzheee..."

Picha za burudani hiyo ya Valentine unaweza kubofya po kwenye mitandao rafiki hapo kwenye Kiluvya pub. Haya sasa bofya hapo chini.

Posted by BM. on Thursday, February 18, 2010


Kibaridi kimeshika leo hapa Tokyo lakini kibarua muhimu wacha twende tu.


Nakaribia mjengoni B/H.
Mdau Reginald Ndesika naye alikuwa njia moja ..aliiona flashi ya kamera..Safi haya twende sasa...

Posted by BM. on Monday, February 15, 2010

Paul, 25, and Ruth Muli, 56, during their wedding at the Rock City Hotel in Nairobi, on Sunday. Photo: Mbugua Kibera /Standard

Kwa hakika J2 iliyopita ya tarehe 14/02 ,Siku ya wapendanao, ilikuwa maalum kwa kijana PAul Muli (25)na Bi. Ruth Wanjiru (54) ,Mfanyabiashara millionea raia wa Kenya walipofunga ndoa baada ya kuwa wapenzi kwa miaka mitatu. Sherehe zilifanyika katika Hoteli ya Rock City Hotel na kuhudhuriwa na wageni takriban 250 ikiwa ni pamoja na watoto wa mama huyu , mtoto wa kiume mwenye miaka 34 na wa kike mwenye miaka 23.Tofauti ya umri imezusha mjadala kuwa ...Eeeh Imekuaje! lakini swali hapa kuna mbaya gani?Unasemaje...
Na huko Nigeria Mwanaume mmoja mwenye miaka 84 anaishi na wake zake wapatao 86 na watoto zaidi ya 150 na wakeze wanampenda ile mbaya. Mahakama ya Kiislamu imemlazimisha awatimue wake zake 82 abaki na wanne na amegoma , hii unaionaje ...ipi kali zaidi.Bofya hapo chini.

Posted by BM. on Sunday, February 14, 2010


Tafakari......!

Posted by BM. on Sunday, February 14, 2010


Watangazaji wa baadaye wanahitaji maandalizi ya mapema...Hongereeni !

Posted by BM. on Sunday, February 14, 2010


Hapo kilimaniinaaminika kuwa ndipo amri kumi za Mungu zilishushwa kwa Mtume Moses
au Nabii Mussa ,Mashariki ya kati. Mahujaji wapo hapo wakifanya ibada ya maombi.

Posted by BM. on Sunday, February 14, 2010

Nguo za kumkinga mtoto na kibaridi...Swali hapa ni kuwa wazazi wake walikuwa wanataka kutuma ujumbe gani...na je mtoto huyo angejua maana yake angekubali kuvaa hivyo vitaulo?

Posted by BM. on Friday, February 12, 2010


Tarehe 14/2 ni siku ya wapendao...siku zinajongea na mengi yataandikwa kuhusu siku hii. Mirindimo , mapema kabisa inawapa 5 wapenzi wake kwa kuichagua kuwa kipenzi chao. Mirindimo iko pamoja nanyi kwa kila hatua.Hebu sasa nikupe zawadi ya Valentine day kutoka kwa Valentina.

Mdada wa Ki-Bulgaria Valentina Hassan akiimba wimbo wa mwanamuziki Mariah Carey "withot you" yeye akiupachika jina la Ken Lee...ni burudani ya aina yake na vipaji vinaonekana.Nawe unaweza kuimba wimbo gani hata wa kuiga...? Hebu tusikie wimbo orijino kutoka kwa mwenyewe Mariah Carey.

Siku Njema....

Posted by BM. on Tuesday, February 09, 2010

pliz, No comment!

Posted by BM. on Tuesday, February 09, 2010

Kuna ukweli kuwa wake wa wapiganaji wana ujasiri fulani katika mienendo na kauli zao. Hili ni jambo lililo na ukweli . Bofya hapo umsikie huyu , mama , kauli zake zinaweza kukufanya umwelewe vizuri.


Mke wa kiongozi wa kwanza wa Sudani Kusini Hayati John Garang , anaitwa bi Rebecca Garang alipokuwa katika mahojiano na Mtangazaji wa Sauti ya Amerika -VOA Shaka Ssali katika kipindi cha Straight Talk Africa , kuhusiana na mume wake. Ushupavu wa mwanamke huyu umenifurahisha sana..

Posted by BM. on Tuesday, February 09, 2010

Waziri Mkuu wa Urussi Vladmir Putin akiwa katika mapumziko; huwa anafanya mazoezi magumu na kazi nzito nzito kama vile yuko vitani. Yuko fit kwa lugha nyepesi. safiii!

Posted by BM. on Monday, February 08, 2010

Kwa wale wasiopenda presha katika mirindimo ya muziki ...kibao hiki kinawafaa. Watu wazima wakipimana sauti. Hayati Madilu Multi Syeteme na Nyboma mwandido,mkongo wa anayeaminika kuwa na sauti tamu ..bofya hapo katikati.

Posted by BM. on Saturday, February 06, 2010


Sio Ntwara peke yake hata Lilongwe, Malawi kitoweo kinachokubalika. Hapa kando ya barabara kuu inayoingia Lilongwe.Bei inategemea jisi alivyonona. Ujasiriamali mbadala!...

Posted by BM. on Saturday, February 06, 2010


Vijana wa Kisomali wakiwa na mateka wao watalii wa kifaransa, waliwateka bahari ya hindi wakiwa na boti yao wakiekea Afrika ya Mashariki.baadaye waliwaachia baada ya kupata kikombozi duh !

Posted by BM. on Saturday, February 06, 2010


Wanajeshi wa Marekani wakiwa vitani nchini Afghanistan , baada ya kutembea bila kupumzika kwa siku sita usiku na mchana huku wastani wa Joto ni digrii za selsiasi 40 . Sasa eneo la kupumzika kila mtu anatakiwa aandae kitanda kwa kuchimba hapo na kulala kwa saa sita kabla ya kuendelea na safari...kazi ipo mkubwa!

Posted by BM. on Saturday, February 06, 2010


wachimbaji wadogo wadogo wa dhahabu katika mgodi wa Chudja Kilomoto kaskazini mashariki mwa DRC wakihangaika kutafuta riziki. Mazingira ya kazi ni magumu na hatari ...lakini mkono azima wende kinywani.

Posted by BM. on Saturday, February 06, 2010


Kiongozi wa Chama cha Upinzani nchini Afghanistan , Abdullah Abdullah aliyeshindwa katika uchaguzi na Raisi Karzai wa nchi hiyo, katika uchaguzi wa utata , aliwa anaongea na vyombo vya habari nyumbani kwake katika jimbo la Bamiyan Kati huko Afghanistan.

Posted by BM. on Saturday, February 06, 2010


Barabara ya kwenda kwetu; Mbulu kwenda Babati...Miundombinu ni tatizo kwetu.Lakini wakati wa kiangazi tunapita hapo raha mustarehe.

Posted by BM. on Saturday, February 06, 2010


Tutafika kwa mtindo huo!

Posted by BM. on Saturday, February 06, 2010


BAE Systems, mojawapo ya makampuni makubwa kabisa duniani ya uundaji wa vifaa vya kijeshi, itatozwa faini ya dola milioni 400.BAE inalipa faini hiyo baada ya kukiri hatia ya kufanya njama ya kuwasilisha taarifa za fedha zenye udanganyifu mbele ya serikali ya Marekani. Vile vile, imekubaliana na Idara ya Upelelezi wa Makosa Mazito ya Ugandanyifu ya Uingereza (SFO), kukiri kuwa na hatia ya kushindwa kutekeleza wajibu wake. Wajibu huo ulikuwa ni kuweka kumbukumbu sahihi za mahesabu katika malipo yaliyofanywa kwa mshauri wake wa masoko nchini Tanzania ili kufanikisha mauzo ya rada ya kuongozea ndege. BAE Systems imeagizwa na idara hiyo ya Uingereza, kulipa faini ya dola milioni 30, ambapo kati ya hizo, kiasi kitapelekwa Tanzania kusaidia shughuli za hisani. Hata hivyo, hatua hiyo ni fedheha kubwa kwa BAE kutokana na kukiri kuwa na hatia ya mashtaka ya jinai Marekani na Uingereza.Ingawa adhabu ya Uingereza inaonekana kuwa ndogo kuliko ile ya SFO iliyokuwa ikitaka, inaaminika kuwa ni rekodi ya kipekee kwa kampuni ya Uingereza kukutwa na hatia ya jinai.
Mashtaka ndani ya Uingereza yanahusiana na kampuni hiyo kuiuzia Tanzania rada ya kuongozea ndege kwa mamilioni ya dola katika mkataba wenye utata uliosaniwa mwaka 1999.(source bbc).

Posted by BM. on Thursday, February 04, 2010


Amini usiamini huyu ni binti wa miaka 13 tu, anaitwa Zara Hartshorn wa nchini Uingereza. Alipatwa na ugonjwa wa ajabu anashindwa kuufaidi utoto wake kutokana na jinsi watu wanavyomchukulia kuwa yeye ni bibi mwenye umri wa miaka zaidi ya 50
Siku moja Zara Hartshorn alipanda basi la abiria na kutaka kukata tiketi ya watoto lakini dereva wa basi hilo alimuangalia kwa mshangao na kumwambia kuwa asifanye masihara alipe pesa kamili.Zara aliposema kuwa yeye ni mtoto na ana umri wa miaka 13, dereva huyo ambaye alikuwa ni mzee wa makamo, alicheka sana na kumwambia kama ndio hivyo basi na mimi nina umri wa miaka 21.Abiria nao waliingia kwenye mjadala huo na kumuunga mkono dereva kuwa Zara anawachezea watu akili kwani anaonekana wazi kuwa yeye ni kikongwe mwenye wajukuu.Zara kwa aibu alishuka toka kwenye basi hilo na kusubiria basi jingine kwa imani dereva wa basi lifuatalo angeweza kumuelewa kuwa yeye ni mtoto.Huo ni mkasa mdogo sana kati ya mikasa inayomkumba binti Zara Hartshorn wa Rotherham nchini Uingereza ambaye umri wake halisi ni miaka 13 pamoja na kwamba anaonekana kuwa na umri zaidi ya miaka 50.Zara anakabiliwa na ugonjwa unaoitwa lipodystrophy ambao humfanya aonekane mzee sana kuliko umri wake huku akiwa na tabia za kitoto kama watoto wenzake.Mama yake Zara bi Tracey Pollard ilibidi achukue uamuzi wa kumsimamisha masomo Zara kwakuwa alikuwa akitaniwa sana na wenzake akiitwa "Bibi" na kubandikwa majina kadhaa ya fedheha.Ugonjwa unaomkabili Zara umewahi kuwatokea watu 2,000 tu duniani ambapo tabaka la chini la mafuta la ngozi hutoweka na kuifanya ngozi izeeke kwa spidi ya ajabu sana.Ugonjwa wa lipodystrophy hauna tiba hivyo Zara ataendelea kuzeeka mapema jinsi anavyozidi kuendelea kukua.Zara amerithi ugonjwa huo toka kwa mama yake ambaye ni miongoni mwa wagonjwa wachache sana duniani wa ugonjwa huo."Nilijuta kumzaa Zara, nilihuzunishwa sana nikifikiria kuwa Zara atapitia matatizo yote yaliyonikumba mimi wakati wa utoto wangu", alisema mama yake Zara.Zara anaelezea masikitiko yake kutokana na jinsi watu wanavyomchukulia na kumtania kwa kusema kuwa wakati mwingine hukimbilia chumbani kwake na kuanza kulia peke yake.Unaweza kufuatilia habari zake zaidi kupitia Video hiyo hapo chini ...Take 5 mtandao wa Nifahamishe.

Posted by BM. on Thursday, February 04, 2010


Wizi wa simu ya mkononi Kwetu Afrika Mashariki ni jambo la kawaida , hata miye niliwahi kuibiwa kwa kuporwa. Sasa inasemekana njia ya kufanya imepatikana; Kwanza kabisaa ukipata simu mpya piga namba ifuatayo; *#06#
utaziona tarakimu 15 zinajitokeza , hebu zinakili namba hizo.
1:Ukiibiwa simu yako tuma kwa njia ya mail hizo namba kwa **
cop@vsnl.net* au * au kwa phone provider wako
2:Your Mobile will be traced within next 24 hrs via a complex system of
GPRS and internet.
3: You will find where your hand set is being operated even in case your
number is changed
KUMBUKA tu ; ni ujumbe , miye sijajaribu lakini nauamini unaweza kujaribu.

Posted by BM. on Thursday, February 04, 2010


Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma amekiri kuwasaliti wake zake watatu na kuzaa na mwanamke mwingine nje ya ndoa.

Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma amezithibitisha taarifa za vyombo vya habari kuwa alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na binti wa rafiki yake na amemzalisha mtoto wa kike.Katika taarifa iliyotolewa na ofisi ya Zuma jana, Zuma amekiri kuwasaliti wake zake watatu na mchumba wake anayetegemea kumuoa hivi karibuni.Mbali na kukiri uhusiano huo, rais Zuma amepinga vikali tuhuma kuwa anaonyesha mfano mbaya wakati harakati za kupambana na ukimwi zikiendelea nchini Afrika Kusini.Asilimia 10 ya raia wa Afrika Kusini wanaishi na virusi vya ukimwi.
Vyombo vya habari vya Afrika Kusini viliripoti wiki hii kuwa Rais Zuma mwenye umri wa miaka 67 amezaa na binti wa rafiki yake wa karibu ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya kombe la dunia nchini Afrika Kusini.Gazeti la Sunday Times la Afrika Kusini liliripoti kuwa Zuma alizisaliti ndoa zake na kuzaa na Sonono Khoza ambaye ni binti wa Irvin Khoza, mmiliki wa timu ya Orlando Pirates.Sonono mwenye umri wa miaka 39 alijifungua mtoto wa rais Zuma mwezi oktoba mwaka jana.Kwa mujibu wa gazeti hilo, baba yake Sonono alielezea kuhuzunishwa sana na kitendo cha Zuma kumtia mimba binti yake.Khoza aliiambia familia yake kuwa anahisi amesalitiwa na Zuma ambaye alikuwa akimchukulia kama rafiki yake wa karibu sana.

Chanzo;AAP

Posted by BM. on Wednesday, February 03, 2010

Rais Abdillahi Yusufu katika mazungumzo tete na Raisi wa Tanzania Jakaya Kikwete wa Tanzania huko Adis Ababa , Ethiopia ambako kulikuwa na Mkutano wa wakuu wa nchi wanachama wa AU.

Posted by BM. on Wednesday, February 03, 2010

Jiji la Tokyo limekuwa baridi hasaaa kwa theluji. Sijui wezetu huko Marekani Kaskazini na nchi za Scandinavia kaskazini mwa Dunia...du poleni sana . Hapa si saaana lakini imo nayo.. Eeh kibaridi kimekolea ..picha hiyo imepigwa kupitia dirishani , nyumba ninayoishi hapa mtaani....duh! Njia ya treni ilipambwa na theluji japo haikuzuia treni kupita...
Muonekana ya bustani ya Yoyogi Koen barafu ilipotulia kudondoka ..
Kijinjia cha kuelekea kibaruani , jengo la utangazaji la NHK-Japani pembezoni kumepambwa na theluji.

Posted by BM. on Wednesday, February 03, 2010


Utafiti wa Mirindimo kupitia ukokotozi unaonyesha kuwa wimbo huu unapendwa sana ..unadhani kwanini...!

Posted by BM. on Monday, February 01, 2010

Barafu inaendelea kudondoka kwa wingi usiku huu(J3) katika jiji la Tokyo na kuifanya hali ya baridi kuwa ya lawama zaidi. Mchana joto ilikuwa digrii 10 ...sasa imefika tatu na inazidi kushuka..bila kikanza hulali..sore kwa lugha nyingine kipashamoto cha nyumba au kwa kisukuma hita.
Kibaridi hadi kunako mfupa!Nje hakukaliki. Kwetu Hale mkeka wakunjwa.

Posted by BM. on Monday, February 01, 2010


DAKTARI wa Hospitali ya Marie Stoppers iliyopo Mwenge, jijini Dar es Salaam, Paul Andrew ametiwa mbaroni kwa tuhuma za kumbaka mgonjwa aliyefika hospitalini hapo kupatiwa matibabu.Taarifa zilizothibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Elias Kalinga zimesema kuwa mgonjwa huyo alifika hospitalini hapo kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi wa tumbo ndipo Dk. Andrew alimwandikia kipimo cha Utra Sound.
Akizungumza na Tanzania Daima jana, Kamanda Kalinga alisema kwa mujibu wa mgonjwa huyo, alifika hospitalini hapo majira ya jioni na baada ya kueleza tatizo lake, Dk Andrew alimwandikia kipimo hicho.Kamanda Kalinga alieeleza kuwa baada ya kuingia katika chumba cha kufanyiwa kipimo, ndipo daktari huyo alimpa kitu kilichomfanya alale kwa muda na nguvu ya dawa ilipokwisha alishtuka na kumkuta daktari huyo akiendelea kumbaka.“Baada ya kumkuta daktari akimbaka, mgonjwa huyo alitoka na kukimbilia Kituo cha Polisi Mabatini kilichopo Kijitonyama na kufungua jalada lenye namba RB/KJN/123/552/10,” alieleza.Alisema askari hao walirudi na mgonjwa huyo hospitali na kumkamata mtuhumiwa aliyekuwa bado yupo eneo hilo.Kamanda alisema mgonjwa huyo amefanyiwa vipimo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ili kubaini kama kweli alifanyiwa unyama huo.Alisema mtuhumiwa bado anashikiliwa na polisi na leo anatarajiwa kupandishwa kizimbani kujibu tuhuma hizo.habari na Betty Kangonga wa gazeti la Tanzania Daima.
(Kama ni kweli imefanyika hivyo)!!!!Huu ni aina ya ugaidi, sijui unasemaje mdau!

Posted by BM. on Monday, February 01, 2010

Timu ya mafarao wa Misri wamelibeba kombe la Africa katika mechi kali iliyofanyika jana huko Angola. Ni mchezaji Mohamed Gebo aliyefunga bao la pekee katika dakika ya 85 na kuiwezesha timu yakle kuchukua kombe hilo kwa mara ya tatu mfululizo . Tayari inakuwa mara saba sasa katika vipindi tofauti kombe hilo kuchukuliwa na tomu hiyo ya taifa ya nchi hiyo. Sasa Nguvu kombe la dunia 2010. Hongereni Mafarao!
Hebu pata fursa ya kuwajua wachezaji wa Misri waliotwaa kombe la Afrika 2010.