Kuna taarifa kuwa Jose Cammellion , mwimbaji kutoka nchini Uganda anayetarajia kuitembelea Japani hivi karibuni amevunjika miguu yote miwili kufuatia kitendo chake cha kujirusha kutoka ghorofa ya tatu ya Hoteli ya Impalla mjini Arusha.
Chanzo cha habari kinataarifu kuwa tukio hilo lilitokea alfajiri ya saa 11 kuamkia juzi.
Sababu ya Camellion kuchukua uamuzi huo haijajulikana na Polisi wanaendelea kuchunguza tukio hilo. Msanii huyo alikwenda Tanzania kwa ajili ya maonyesho ya Fiesta ya Tanga chini ya udhamini wa Clouds FM na sasa amelazwa hospitalini , kampala baada ya kuchukuliwa na baba yake kwa ndege maalum kwenda kampala , Uganda.. Hali hiyo ilimfanya ashindwe kufanya shoo huko Tanga ambako wasanii wengi wa Tanzania walialikwa na yeye ndiye alikuwa mgeni maalum mwongozaji wa tamasha. Hata hivyo tamasha hilo lilifanyika bila Camellion.
Bado kuna wasiwasi mkubwa ikiwa Camellion atakuja hapa Japani kwa ajili ya onyesho la tarehe 19 , October kama ilivyopangwa.
Ni hapa...
Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!
Posted by
BM.
on
Monday, October 06, 2008
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

0 comments:
Post a Comment