Ni hapa...

Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!

Posted by BM. on Friday, October 31, 2008


Huyu Jamaa (Kulia) anaitwa Generali Laurent Nkunda , mhitimu wa Chuo Kikuu masuala ya saikolojia ndiye anayeongoza vita kikosi cha waasi huko DRC.
Umoja wa Mataifa umesema una wasiwasi na hali za maelfu ya watu wanaoukimbia mji wa Goma. Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa mbali na kulaani ghasia hizo limemtaka kiongozi wa waasi kutekeleza uamuzi wake wa kusimamisha mapigano.
Watu wengi waliokimbia mapigano hayo kwa sasa wanaishi katika majengo ya shule, makanisa na wengine wanalala nje. Jana Alhamisi Kiongozi wa waasi wa CNDP Laurent Nkunda, ambaye wapiganaji wake wapo nje kidogo ya mji wa Goma, ametangaza kusimamisha mapigano na kuzitaka pande nyingine zinazohusika na mzozo huo kufanya hivyo pia. Hebu fuatilia picha nyingine za machafuko hayo.

0 comments: