Kuna taarifa kuwa Tabu ley amelazwa hospitalini kwa tatizo ambalo halijajulikana bado lakini inaonekana kama kiharusina hali yake si nzuri sana.
Habari za kupooza kwa kiongozi huyo wa Kundi la muziki la ‘Orchestre Afrisa International’ zilitolewa na mmoja wa wanamuziki wa kundi hilo kwa vyombo vya habari nchini humo kupitia mtandao.Taarifa hiyo ilisema kuwa Tabu Ley alilazwa katika Hospitali ya St. Luc’s iliyopo jijini Brussels nchini Ubeligiji akisumbuliwa na ugonjwa ambao haukutajwa jina.Tabu Ley ni Mwanamuziki huyo amewahi kushika nyadhifa mbalimbali katika serikali ya DRC kama vile Uwaziri na Kaimu Gavana wa Jiji la Kinshasa
0 comments:
Post a Comment