Yaani Obama kweli !...
Raisi Mteule wa Marekani hivi majuzi aliwashangaza watu baada ya kuingia katika mitaa ya Washington kupata chai na kitafunwa ..Aliibuka ghafla katika mgahawa mmoja wa vyakula vya bei poa vya "Fast food" jijini Washington na kukaa na wateja wengine wa kawaida na kupata chai na hamburger moja.Akiwa kwenye mgahawa huo unaoitwa Ben's Chilli Bowl uliokuwa na bango kubwa lililosomeka "Hapa Bill Cosby peke yake ndio anaweza kula bure" , Obama alipiga story na wateja wengine huku wengine wakitumia nafasi hiyo kumpiga picha na wengine kupiga naye picha.Baada ya kumaliza kula, Obama alitakiwa kulipa dola 12 na senti 55 lakini Obama alitoa dola 20 na kumwaambia jamaa kip chenj..
Ni hapa...
Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!
Posted by
BM.
on
Tuesday, January 13, 2009
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment