Ni hapa...

Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!

Posted by BM. on Monday, January 19, 2009


Mke wa rais wa Zimbabwe Grace Mugabe amempa kipondo mpiga picha toka Uingereza alipojaribu kumpiga picha ya karibu wakati mke huyo wa rais alipokuwa likizo nchini Hong Kong kumtembelea binti yake.
Mpiga picha huyo toka Uingereza amelalamika kuwa mke wa rais wa Zimbwabwe alimpiga magumi ya uso mara kibao alipojaribu kumpiga picha karibu na hoteli moja ya kifahari jijini Hong Kong.Richard Jones aliliambia shirika la habari la Associated Press kuwa Grace Mugabe, 43, aliwaamuru walinzi wake wamkamate mpiga picha huyo na kumshika kwa nguvu wakati mke huyo wa rais alipokuwa akitoa kipondo kwa mpiga picha huyo."Alinitandika ngumi kadhaa usoni" alisema Jones. "Alikuwa amevaa pete ya almasi ambayo ilinisababishia majeraha kadhaa usoni".Jones, 42, kutoka Machen kusini mwa Wales, alikuwa Hong Kong kwaajili ya gazeti la The Sunday Times lenye makazi yake London, Uingereza.Jones alisema kuwa ngozi ya uso wake ilipata mipasuko zaidi ya 10 ingawa hakuhitaji kupelekwa hospitali.Msemaji wa polisi wa Hong Kong Odelia Tam alisema kuwa polisi wanachunguza mkasa huo na kwamba hadi sasa hakuna aliyekamatwa.Ubalozi wa Zimbwabwe Beijing ulikataa kujibu simu zote zilizokuwa zikitaka ufafanuzi wa suala hilo.Mke huyo wa rais wa Zimbwabwe alikuwa Hong Kong kumtembelea binti yake Bona anayesoma nchini humo.Inasemekana Grace Mugabe aliondoka Hong Kong baada ya mkasa huo wa kumpa kisago mpiga picha huyo.

0 comments: