Ni hapa...

Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!

Posted by BM. on Tuesday, January 13, 2009

Benki kuu ya Zimbabwe imezitangaza noti mpya za dola ya Zimbabwe bilioni 20 na noti zingine za dola ya Zimbabwe bilioni 50 katika gazeti la Herald la nchini humo.Benki kuu ya Zimbwabwe imekuwa ikitoa noti mpya kila bei za vitu zinavyozidi kupanda juu. Mwezi disemba Benki hiyo pia ilitoa noti mpya za dola ya Zimbabwe bilioni 10.Kutokana na kuyumba kwa uchumi wa nchi hiyo biashara nyingi nchini humo zinafanyika kwa kutumia dola ya Marekani au Rand ya Afrika Kusini.Kabla ya benki kuu ya Zimbwabwe kufuta sifuri 10 katika noti zake, noti kubwa kuliko zote kuchapishwa ilikuwa dola bilioni 100 mwezi wa nane mwaka jana. Baada ya sifuri hizo kufutwa gazeti la Herald nchini humo lilikuwa likiuzwa dola 10 za Zimbwabwe.Gazeti hilo hilo hivi sasa linauzwa dola bilioni 15 za Zimbwabwe.Uchumi wa Zimbwabwe umekuwa ukiyumba kutokana na migogoro ya kisiasa inayoendelea nchi humo hali iliyosababisha uhaba wa chakula, mafuta na umeme. Matatizo ya maji pia yamechangia kufumuka kwa ugonjwa wa kipindupindu ambao hadi sasa umeishaua zaidi ya watu 2000.

0 comments: