Ni hapa...

Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!

Posted by BM. on Sunday, January 25, 2009


Mrembo wa Brazili aliyekuwa aiwakilishe Brazili kwenye Miss World ambaye alikatwa mguu na mkono ili kuzuia kusambaa kwa ugonjwa uliokuwa ukimkabili amefariki dunia.
Mrembo huyo mwenye umri wa miaka 20 ambaye alikuwa aiwakilishe Brazili kwenye mashindano ya urembo wa dunia, amefariki pamoja na kukatwa mkono na mguu ili kuzuia kusambaa kwa ugonjwa aliokuwa nao.Mariana Bridi da Costa alikatwa mkono na mguu katika jitihada za madaktari kuzuia kusambaa kwa bakteria waliotokana na maambukizi katika njia ya mkojo na kusababisha ugonjwa wa septicaemia.Madaktari walisema hali ya mrembo huyo ilizidi kuwa mbaya majira ya usiku na mrembo huyo alifariki asubuhi.Ugonjwa wake ulikuwa ukisababishwa na bakteria Pseudomonas aeruginosa ambaye anajulikana kuwa ni sugu kwa madawa mengi.Bridi alizidiwa mwezi wa disemba na kupelekwa hospitali ambapo madaktari walimwambia anasumbuliwa na mawe kwenye figo kabla ya kulazwa tarehe 3 mwezi huu katika hospitali moja kusini mashariki mwa Brazili.Rafiki wa kiume wa binti huyo, Thiago Simoes, alisema kuwa Bridi alizidiwa disemba 30 lakini madaktari walimwambia anasumbuliwa na mawe kwenye figo.Maambukizi yaliendelea kwenye mwili wake na kumsababishia kuzidiwa na kupelekwa hospitali kwa uchunguzi zaidi ndipo ukweli wa mambo ulipojulikana.Iliwabidi madaktari kukata mkono wake na mguu wake ili kuzuia kusambaa kwa ugonjwa huo.Bridi aliwahi kufikia fainali mara mbili katika mashindano ya urembo kuwania mwakilishi wa Brazili kwenye Miss World.

0 comments: