Ni hapa...

Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!

Posted by BM. on Friday, February 13, 2009

Visanamu ...akiviangalia kuchagua shepu anayotaka ;
SASA; Michael Jackson amepatwa na ugonjwa wa ajabu unaofanana na ugonjwa wa MRSA ambao unatafuna nyama za ndani ya mwili.Hivi sasa Michael Jackson mwenye umri wa miaka 50 amewekewa dripu ya antibiotics katika jitihada za kupambana na virusi vya ugonjwa huo wa ajabu ambavyo inasemekana vimeenea sehemu kubwa ya mwili wake.Mwanamuziki huyo alionekana akiwa na ngozi kama ya mtu aliyeungua moto kwenye uso wake na mikono yake wakati alipoenda zahanati ya Beverly Hills wiki hii.Gazeti la The Sun la Uingereza lilidai kwamba Michael Jackson alipata maambukizi ya virusi hivyo wakati alipokuwa akifanyiwa marekebisho ya pua yake mwezi uliopita.Chanzo kimoja kililiambia gazeti hilo kwamba "Michael Jackson aliambukizwa maambukizi ya ajabu wakati alipokuwa akifanyiwa upasuaji wa kurekebisha pua yake mwezi uliopita"."Ugonjwa wenyewe unafanana na MRSA kwakuwa na wenyewe ni sugu kwa antibiotics za kawaida hali iliyopelekea Michael Jackson kuwekewa dripu ya antibiotics"."Maambukizi yameenea kwenye uso wake na mwili wake na yamekuwa yakienea kwa kasi sana"."Kuna uwezekano ukageuka kuwa ugonjwa unaonyofoa nyama za ndani kwani umeishaanza kunyofoa ngozi yake na madaktari wanampa matibabu kwa uangalifu mkubwa".Mwezi disema mwaka jana uvumi ulisambaa kwamba Michael Jackson ana matatizo makubwa ya mapafu lakini msemaji wa Michael Jackson alikanusha uvumi huo.

0 comments: