Ni hapa...

Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!

Du!

Posted by BM. on Thursday, February 19, 2009


Mwanaume mmoja mwenye wivu amemuua mkewe baada ya mkewe kutaja jina la mwanaume mwingine wakati wakifanya tendo la ndoa. Colin Scully,53 amepandishwa kizimbani kwenye mahakama ya Leeds, Uingereza baada ya kumuua mkewe Tracey,39 kwa kumniga koo lake kutokana na wivu baada ya mkewe kutaja jina la mwanaume mwingine wakati wanafanya mapenzi.
Inasemekana kwamba Colin alikuwa akishuku mkewe anatoka nje ya ndoa baada ya kufanikiwa kusoma ujumbe wa simu katika simu ya mkewe lakini akaamua kufanya uchunguzi wake kimya kimya.Pamoja na jitihada zake Colin hakufanikiwa kupata ushahidi wa kuthibitisha kutoka nje kwa mkewe.Inasemekana usiku mmoja wakati wanafanya tendo la ndoa mkewe kwa bahati mbaya akamwita mumewe "Paul" jina la mwanaume mwingine.
Paul hakuwa mwingine bali ni Paul Daigton rafiki wa mkewe ambaye wako pamoja katika klabu yao ya scooter.Colin kwa hasira alimkamata mkewe shingoni na kumkandamiza kwa nguvu kwa muda mpaka alipoona mkewe hatingishiki na kumuacha na kwenda kulala chumba cha watoto wao.Inasemekana kwamba asubuhi wakati Colin akijiandaa kwenda kazini ndipo alipogundua kwamba alimuua mkewe na kuamua kupiga simu polisi "Nimemfanyia kitu mke wangu, sijui nimefanya nini".
Polisi walipofika eneo la tukio walimkamata Colin na baada ya maiti kufanyiwa uchunguzi iligundulika kwamba marehemu alifariki baada ya kukandamizwa shingoni kwa muda mrefu.Kesi yake itaendelea kusikilizwa kwenye mahakama hiyo. imekaaje hii..

0 comments: