Jumamosi Feb.14 ni Siku ya WAPENDANAO. Mambo mengi yanafanyika siku hiyo dunia nzima huifurahia siku hii na jambo lililozoeleka siku hizi kwa wapenzi ni kutoka Out kwa raha zao na bila shaka kubadilishana zawadi ya viwango tofauti.
Vivazi vyekundu na maua mekundu imekuwa fasheni siku hizi katika hafla za siku ya wapendanao na inapendeza.
Wakati haya yakifanyika ni fursa nzuri pia kutafakari . Naamini utakuwa na muda huo ikiwa uko makini . Hivyo kwa yule aliye makini ana mahali pa kuanzia kufikiri juu ya mpenzi wake.
Hebu jiulize je kila unachokifikiri , unachokiamini, unachokipenda, unachokishabikia , unachoking’ang’ania ama unachokiendekeza ni ‘sahihi tu’ hata kama kinaangaliwa tofauti na mwenzi wako?.
Wapenzi walio na tabia ya kuvuta kamba sana mwishowe hujikuta katikati ya ule usemi majuto mjukuu.Valentine huwa siku ya manufaa kwa watu wanaojifunza na wanaokubali kuyatumia kwa kuyaamini maneno yafuatayo; nakupenda, nakuamini, pole, samahani, ndio na nimeelewa.
Ni mara ngapi umeshajisikia ugumu kuyatumia maneno hayo kwa yule umpendaye? .
Hasira, ugonvi, visa , vitimbwi , tambo na kejeli kwa mpenzi wako wa kweli zinaanzia wapi!. Usiogope kujiuliza na kujipa majibu sahihi.Nadhani wakati huu unapoanza kujadili kile ulichokisoma utakuwa umeanza kusherehekea siku ya wapendao, . Unasemaje!
Dira Ya Dunia
2 hours ago
0 comments:
Post a Comment