Ni hapa...

Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!

Posted by BM. on Wednesday, February 25, 2009

Madaktari wanapokata tamaa........
Nyota wa vipindi vya televisheni Uingereza, Jade Goody ambaye aliolewa mwishoni mwa wiki baada ya madaktari kumwambia kuwa ana siku chache za kuishi kutokana na saratani yake kufikia pabaya amesema kwamba sasa yuko tayari kuelekea peponi.
Jade alifunga ndoa na mpenzi wake Jack Tweed katika harusi iliyofana sana mwishoni mwa wiki ikiwa ni siku chache baada ya madaktari kumtaarifu Jade kwamba kansa yake imefikia hali mbaya na kwamba nyota huyo ana wiki chache tu za kuishi kabla hajafariki.
Jade alizikusanya nguvu zake zote na kufanikiwa kusimama na kudansi kwenye harusi yake pamoja na hali yake kuzidi kuwa mbaya.Mume wa Jade, Jack Tweed ambaye bado anatumikia kifungo cha nje akitakiwa kuwa nyumbani kwa familia yake kabla ya saa moja usiku kila siku, alipewa idhini maalumu na Jack Straw kutumia usiku mmoja wa harusi yake na mkewe.Jack Tweed alifungwa miezi 18 mwaka jana baada ya kumshambulia kijana mmoja wa miaka 16 na gongo la mpira wa gofu, lakini sasa ametolewa jela akiendelea kutumikia kifungo chake nje.Jade, mama wa watoto wawili alishindwa kabisa kuficha huzuni yake aliporudi nyumbani kwake akiwa anatokwa na machozi huku akisaidiwa kutembea na mumewe na msaidizi wake.
"Amechoka sana , harusi ilikuwa nzuri sana lakini imemfanya achoke zaidi" alisema mama yake Jackiey Budden."Nilifanikiwa kutumia siku yenye furaha zaidi kuliko zote katika maisha yangu" Jade aliliambia jarida la OK! na kuongeza kwa kusema kuwa "Sasa nipo tayari kuelekea peponi".Jade aliuza hati miliki za harusi yake kwa paundi milioni 3 ambazo alisema ataziweka katika mfuko wa kuwatunza wanae wawili Bobby,5, na Freddy, 4.Jade aligundulika ana saratani wakati alipokuwa akishiriki Big Brother ya India inayojulikana kama Big Boss mwaka 2008.Jade alirudi Uingereza na kuanza matibabu katika hospitali ya Royal Marsden Hospital iliyopo jijini London.
Jade aliamua kufunga ndoa na mpenzi wake Jack Tweed siku chache baada ya kuambiwa atafariki katika wiki chache zijazo kwakuwa ugonjwa wake umefikia hatua ambayo hauwezi kutibibika tena. Fuatilia picha hizi Jade akiwa katika hali ya kawaida mitaani…hadi sasa akisubiri siku ya kifo chake…ni ngumu ! unasemaje …Fuatilia picha zake

0 comments: