Waziri wa fedha wa Japani Soichi Nakagawa *Kushoto* amejiuzulu kufuatia kashfa ya kulewa akiwa katika mkutano na waandishi wa habari. Kulia ni boss wake waziri mkuu Taro Aso.
Shoichi Nakagawa ameamua kujiuzulu baada ya shinikizo la kujiuzulu kufuatia kutinga katika kikao cha mataifa makubwa G7 kilichofanyika nchini Italia akiwa amelewa.
Bwana Nakagawa aliomba radhi kwa kuisababishia nchi aibu hiyo na kuwaambia waandishi wa habari kwamba ilikuwa bora kwa yeye kujiuzulu.Hatahivyo Nakagawa alisema kwamba hakunywa sana kama alivyodhaniwa ila alionja kidogo tu.Katika kikao hicho kilichofanyika Roma nchini Italia bwana Nakagawa alikuwa akitoa sauti za kilevi wakati akijibu maswali ya waandishi wa habari huku macho yake yakijifungafunga mara kadhaa.Katika kuonyesha kuwa waziri huyo alikuwa chakari, alikuwa akijibu maswali aliyoulizwa gavana wa benki ya Japan akidhania ameulizwa yeye.Katibu wa chama cha DP Japan Yukio Hatoyama alionyesha hasira zake kutokana na tukio hilo na kusema limeidhalilisha nchi.Nakagawa alisema mwanzoni kwamba hatajiuzulu hadi pale bunge la Japan litakapoidhinisha bajeti.Waziri huyo ilimbidi aachie ngazi mapema baada ya shinikizo la kumtaka aachie ngazi mara moja kuzidi.Waziri mkuu wa Japan Taro Aso alikubali kujiuzulu kwa waziri huyo na kusema kuwa anaheshimu maamuzi yake. Waziri wa Uchumi ameteuliwa kushika nafasi ya waziri huyo.Kujiuzulu kwa Nakagawa kumeonekana kama pigo kwa serikali ya bwana Aso wakati ikijiandaa na uchaguzi ujao.
Mkutano wa TAMSTOA waibua changamoto za Malori
18 minutes ago
0 comments:
Post a Comment