Wanawake wawili wako taabani baada ya sindano walizopigwa ili wawe na matako kama ya Jennifer Lopez kuwasababishia kufeli kwa figo na viungo vingine vya ndani.
Wanawake wawili wanapigania maisha yao baada ya sindano walizopigwa ili wawe na matako kama ya Jennifer Lopez kuwasababishia kufeli kwa figo na viungo vingine vya ndani.
Figo la Andrea Lee, 30, limefeli kabisa baada ya kupata sumu inayosemekana inatokana na silicone inayotumika viwandani.Rafiki yake Zakiya Teagle, 33, yupo mahututi katika hospitali moja Florida baada ya viungo vyake kadhaa vya ndani kusimama kufanya kazi.
Polisi wa Tampa, Florida, wameanza msako mkali kuwatafuta madaktari feki waliowachoma sindano hizo wanawake hao.Sharhonda Lindsay, 32, anatafutwa na polisi baada ya kukimbia alipoona wanawake hao wakikimbizwa hospitali kufuatia sindano alizowachoma.kwa mujibu wa taarifa za polisi, Lindsay, ambaye alikuwa hana leseni yeyote ya utabibu na hana uzoefu wowote wa matibabu ya urembo aliwachoma sindano hizo wanawake hao nyumbani kwake mwezi uliopita. Wanawake hao walizidiwa na hali zao kuwa mbaya sana masaa machache baada ya kuchomwa sindano hizo.
Ms Lee na Ms Teagle walilipa zaidi ya dola 450 ili wapigwe sindano hizo kwa matumaini zingewapa umbile na ukubwa wa matako kama ya J-Lo. Marafiki wa wanawake hao walisema kwamba wanawake hao walikuwa na nia ya kupata umbile na ukubwa wa matako kama ya mwanamuziki Jennifer Lopez ambaye ni maarufu kwa umbile lake hilo.
Polisi walisema kwamba wanawake hao waliambiwa kwamba watachomwa sindano yenye silicone inayoitwa "Hydrogel".Lakini polisi wanafikiria wanawake hao walichomwa sindano iliyokuwa na silicone kali inayotumika viwandani.Polisi wamewataka wanawake kwenye maeneo ya Tampa kujitokeza kama wana taarifa zozote za Lindsay.
EWURA KUBORESHA MAZINGIRA YA WEKEZAJI WA CNG NCHINI
46 minutes ago
0 comments:
Post a Comment