Ni hapa...

Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!

Posted by BM. on Sunday, February 15, 2009

Mwanamama huyu wa Ki-Marekani Nadya Suleman wiki mbili zilizopita alijifungua mapacha wanane kwa mpigo. Picha hii inaonyesha mimba yake zikiwa zimebaki siku nane kabla ya kujifungua. Hii nii mimba yake ya pili mimba yake ya kwanza alijifungua mapacha 6 kwa mpigo.
Kwa hiyo kwa kuzaa mara mbili ana watoto 14 na wote wako katika hali nzuri kabisa .
Anasema kuwa miaka minane kabla ya kujifungua hakuwahi kufanya mapenzi na mwanaume yeyote.
Nadya Suleman, mwanamke aliyejifungua watoto mapacha wanane nchini Marekani ameanza kutoa siri zake kwa kudai kwamba alikaa miaka minane kabla ya kujifungua bila kufanya mapenzi na mwanaume yeyote.Nadya alipata mimba aliyojifungua mapacha hao nane baada ya kupandikizwa mbegu za kiume kutoka kwa mwanaume asiyejulikana ambaye miaka ya nyuma aliwahi kuchangia mbegu zake za kiume katika hospitali ambayo Nadya alijifungua.Hospitali iliyompandikiza mbegu hizo za kiume imekuwa ikilaumiwa kwa kumfanyia matibabu hayo mwanamke huyo aliyekuwa tayari ana watoto mapacha sita.
Nadya mwenye umri wa miaka 33, hakuwahi kufanya kazi alikuwa akiishi kutokana na msaada toka serikalini.Nadya amekuwa akilaumiwa kwa kugeuza watoto wake kuwa mtaji wa biashara kiasi cha kumlazimu kupewa ulinzi baada ya watu wasiojulikna kumtumia vitisho vya kumuua. Wakati Watoto wake wawili wakiwa wamepata wadhamini wa kuwalea, msaada aliokuwa akichukua kutoka serikalini nao umeongezeka kutokana na idadi ya watoto kuongezeka.
Hivi sasaNadya pia amefungua tovuti yake maalumu ili kuwachangisha watu pesa za kumsaidia kulea watoto wake hao.Siku nane kabla ya kujifungua Nadya alipiga picha za mimba yake ambazo zilitoka kwenye vyombo vya habari wiki hii. Haikujulikana Nadya alilipwa kiasi gani ili kupigwa picha hizo. Haijulikani mara ya tatu atazaa wangapi. Take faiv mamaa!

0 comments: