Mwenyekiti mpya wa Umoja wa Afrika AU na ambaye pia ni Kiongozi wa Libya kanali Muammar Gaddafi amedai kwamba maharamia wa Somalia hawafanyi kosa lolote wanapoteka meli za mizigo bali wanatumia haki yao kujilinda kutokana na uvamizi wa meli za mataifa ya magharibi yenye uchu.
Kiongozi wa Libya kanali Muammar Gaddafi amewatetea maharamia wa Somalia kwamba wanatumia haki yao ya kujilinda kutokana na mataifa ya magharibi yenye uchu.Gaddafi aliyasema hayo wakati alipoyatembelea kwa mara ya kwanza makao makuu ya umoja wa Afrika yaliyopo jijini Addis Ababa tangia kuchaguliwa kuwa mwenyekiti mpya wa umoja huo.Gaddafi aliwasili makao makuu hayo akiwa amevalia shati la rangi rangi lililokuwa limepambwa na picha za waasisi wa umoja wa Afrika kama vile Mwalimu J.K Nyerere wa Tanzania Haile Selassie wa Ethiopia, Jomo Kenyatta wa Kenya na Kwame Nkrumah wa Ghana.Kanali Gaddafi alisema kwamba haamini kama maharamia wa Somalia wanafanya kosa lolote.“Ni majibu tosha kwa mataifa ya magharibi yenye uchu ambayo yalivamia na kutumia rasilimali za maji za Somalia kinyume cha sheria" alisema Gaddafi."Wasomali hawafanyi uharamia bali wanajilinda na kulinda chakula cha watoto wa Somalia" Gaddafi alizidi kudokeza.Gaddafi alisema kwamba nchi nyingi hasahasa za magharibi zimekuwa zikijipenyeza kwenye mipaka ya maji ya somalia kinyume na sheria za kimataifa kwakuwa Afrika haina zana za kisasa za kuwafukuza."Kwakuwa Wasomali wameamua kujibu mapigo na kudai haki zao na kulinda rasimali zao zisitumike vibaya, nchi za magharibi zimeamua kuita kitendo hicho "Uharamia"." alisema.Gaddafi alisema pia kwamba yuko katika jitihada za kuwashawishi viongozi wengine wa Afrika kudai fidia kutoka kwa wakoloni kwa mauaji waliyofanya na rasilimali walizoiba wakati wa ukoloni.Alidokeza pia kwamba kuanzia wiki hii Libya itadai fidia ya dola milioni 250 kwa mwaka katika kipindi cha miaka 20 kama fidia toka kwa mkoloni wao Italia ambaye aliitawala nchi hiyo. Gaddafi alidai kwamba bunge la Italia limekubali kulipa fidia hiyo.
Ni hapa...
Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!
Posted by
BM.
on
Saturday, February 07, 2009
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment