Ni hapa...

Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!

Posted by BM. on Wednesday, February 18, 2009


UTATA ulizuka kwa wanaume wawili kila mmoja kutaka kuzika mwili wa mkewe mara baada ya muda mfupi kufariki kwa mwanamke mmoja jijini Dar es Salaam
Utata huo ulizuka jana maeneo ya Tandale Magharibi, baada ya wanaume wawili mmoja aitwae Abdul na mwingine Salum kugombania maiti ya mwanamke mmoja aitwae Tausi Hassan [36] kila mmoja akidai alikuwa mkewe akitaka kwenda kuuzika.Zogo hilo lilizuka baada ya Tausi pamoja na mwanae aitwae Faim Salum kufariki dunia baada ya marehemu na mwanae wakiwa kwenye bajaji kugongwa na gari la taka eneo la Magomeni Mapipa.Inadaiwa na ndugu wa karibu wa mume wa kwanza wa marehemu kuwa, wakiwa nyumbani kwa mume wa marehemu wakijitayarisha na taratibu za mazishi walijitokeza wanawake wapatao watano wenye asili ya kiarabu wakidai wapewe miili yote miwili Tausi na mwanae waende kuizika.Inadaiwa na vyanzo vya habari hizo kuwa, ilibidi ndugu wote waliokuwa mahali pale wapate na mshangao mkubwa na ndipo walipowauliza wao ni kina nani na ndipo walipojitambulisha kuwa wao ni ndugu zake na mume wake marehemu.Na kusema aliyefariki ni mkwe wao na mtoto pia ni wao kwani marehemu alizaa na mtoto wao Abdul ambaye walioana naye mwanzoni mwa mwaka jana.Ndipo ndugu waliopo mahali pale walipotaka wathibitishe kauli za wakina mama hao na kuwataka watoe hati ya ndoa kuonyesha kwamba mtoto wao alimuoa marehemu Tausi.Katika kitu ambacho hakuna mtu ambaye alitegemea mahali pale wakinamama hao walitoa cheti cha ndoa kinachoonyesha Abduli na Tausi walifunga ndoa huko Kariakoo Mtaa wa Jangwani jijini Dar es salaam.Mara baada ya kutolewa kwa vyeti hivyo ndugu wote waliopo msibani hapo walizidi kuchanganyikiwa na mume wa kwanza wa marehemu ambaye ndio alikuwa akijulikana hakukubaliana na watu hao na ndipo sakata hilo lilipozidi kuwa kubwa hadi kutaka kufikishana polisi kuhusiana na suala hilo.Lakini kutokana na tukio hilo ndugu wa marehemu waliona bora wao ndio washuhulike na kuuzika mwili huo kuliko kuendelea na zogo hilo ambalo halikujulikana lingeisha lini.Ndugu wa marehemu waliuchukua mwili huo na kwenda kuzika kijijini kwao Tungi Mkoani Morogoro.Inadaiwa kuwa marehemu alifunga ndoa na wanaume wawili bila mume wake wa kwanza kutambua hilo.Inadaiwa kuwa kwa mara ya kwanza marehemu alifunga ndoa na Salum Senela mwaka 1998.Pia mwanzoni mwa mwaka jana marehemu ilidaiwa kafunga tena ndoa na Abdul hapahapa jijini Dar e salaam.Inadaiwa marehemu alikuwa anaweza kuzimiliki ndoa hizo mbili bila wasiwasi na alikuwa anawapa zamu wanaume hao bila kutambua kinachoendelea.Jamii na ndugu zake marehemu wamesikitishwa sana na tukio hilo kwa kuwa walikuwa hawafahamu kama alikuwa na waume wawili na ajali hiyo ya gari ndio iliyosababisha yajulikane yote hayo.

0 comments: