Binti mrembo wa Kijapani , mwenye sura ya aibu kidogo na kwa muonekano wa nje asiye na rabsha yoyote . Huyu ni Hatakeyama mwenye miaka 34,amehukumiwa kifungo cha maisha jela nchini Japani kwa kumuua mtoto wake mwenye miaka tisa aitwaye Ayaka kwa kumtupa mtoni eneo la darajani.
Ilikuwa tarehe 9 mwezi April mwaka 2006 alimchukua binti yake anayenekana pichani kwenye gari katika mji wa Fujisato mkoa wa Akita na kwenda naye hadi kwenye daraja moja na kumuongopea kuwa anataka kumuonyesha mchezo Fulani. Akampandisha juu ya kingo za jaraja na kumsukumiza.
Kama hiyo haitoshi May 17,2006 alimuua mtoto wa jirani yake ambaye alikuwa akifika mara kwa mara hapo nyyumbani kumuulizia kwa lengo la kutaka kucheza naye. Hatakeyama akaripoti Polisi kwa kudai mtoto alimponyoka alipomuweka katikakingo za daraja lakini wapelelezi hapa wako makini wakagundua kila kitu bila hata kutumia kipigo kama kule…Alipohojiwa sana akadai kuwa ugumu wa maisha ulimchaganya . Mara kadhaa alikuwa akitokwa na machozi mahakamani. Na katika tukio lililowafanya wapelelezi wastuke alisema kuwa muda mfupi kabla ya kumponyoka mwanawe alimwambia mama usiniue …hee akasema amemponyoka …lakini baadaye akasema ..kweli nilimsukuma. Mwili wa mtoto wake umepatikana ndani ya maji na wa jirani pia umeonekana. Hakimu kamwambie akaishi jela MAISHA.
Ni hapa...
Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!
Posted by
BM.
on
Wednesday, March 25, 2009
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment