Ni hapa...

Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!

Posted by BM. on Sunday, March 22, 2009

Shirika moja la Marekani limefanikiwa kutengeneza gari la kwanza duniani ambalo lina uwezo wa kutembea barabarani na kupaa angani kama ndege.Gari-ndege hilo linalouzwa kwa dola 194,000 linatumia mafuta ya kawaida kama magari mengine na lina uwezo wa kubeba abiria wawili tu, gari hilo lina uwezo wa kwenda mwendo wa kilomita 82 kwa saa liwapo ardhini na lina uwezo wa kwenda kilomita 185 kwa saa liwapo angani.Mnunuzi wa gari hilo anatakiwa kuwa na leseni mbili, moja ya udereva wa gari na nyingine ya urubani na ukitaka utapewa mafunzo na urubani kwa watu wanaovutika kununua gari hilo. Gari hilo lina ukubwa sawa na magari mengine kiasi cha kuwa na uwezo wa kuingia kwenye depo ya magari bila matatizo yeyote. Ili kulitumia gari hilo kama ndege, kuna kitufe maalumu ambacho hubonyezwa na kufanya mabawa yachomoze pembeni na ukitaka kulitumia tena barabarani mabawa hujikunja na kuelekea juu.

0 comments: