Ni hapa...

Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!

Posted by BM. on Saturday, March 28, 2009

Tetemeko kubwa limepiga chini ya ardhi km zipatazo 17 katika kisiwa cha Java huko Indonesia karibu na moja ya jiji kubwa nchini humo lenye watu wengi la Yogyakarta

. Palikuwa hapatoshi. Darasa hili ni kwa wasomaji wa Blog hii wanaoishi katika maeneo ya matetemeko hususan nchini Japani.
Hii ni nchi yenye matetemeko mengi, ikiwa wewe unakaa Japani lazima uwe na taarifa juu ya nini cha kufanya pindi balaa hilo likitokea. Kwanza , usitaharuki sana. Mtangulize Mungu na kuwa mtulivu. Kama huna dini endelea na hatua inayofuata. Ukiwa nyumbani hatua ya kwanza kimbilia chini ya Meza ambayo si ya kuunga unga . Maana nyingine zinagawanyika. Usimsahau mumeo , mkeo ,watoto ama mpenzio hakikisha unakuwa naye wakati huu wa taharuki.
Kuna maadalizi ya mapema kabisa. Jiandae kuwa na begi la huduma ya kwanza. Weka dawa ndogo ndogo za maumivu, maji ,tochibetri, Radio ndogo mishumaa, kibiriti na vyakula vya makopo.Lazima ujue kwa hakika nyaraka zako muhimu umeziweka wapi kama vile passport, kitambulisho chako, simu ya mkononi na fedha taslimu. Usiache vitu milangoni kwasababu vinaweza kukandamiza mlango na jiefushe kuweka vitu vizito kwa kuvipanga kwenda juu na kama umefanya hivyo vipange vizuri.
Hakikisha unaondoa plugs zote mara baada ya matumizi ili kuepuka mlipuko. Weka nafasi kati ya vitu vinavyokaribiana na vilipuzi.Maeneo mengi ya Japani kuna maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya kukimbilia watu wakati wa tetemeko na kama ni mgeni angalia wenyewe wanakimbilia wapi. Tetemeko ni tukio la kushitukiza kwahiyo hata unapotembea barabarani lazima uwe na uchaguzi mitaa ya kupita labda ikiwa hakuna budi. Kama huna mahali pa kuingia chukua mto ama nguo weka kichwani utakusaidia bila shaka. Mtikisiko mkubwa unapopita zima majiko ya gesi na vifaa vya umeme .Fungua milango na vaa viatu muda wote unaweza kukatwa na vioo vinavyovunjika.
La msingi usibabaike tetemeko lenyewe halilipuka linatingisha. Epuka kutumia lift kwenye majengo . Tembea usitumie gari, baiskeli wala pikipiki.Mara nyingi nchini Japani Matangazo kwa njia ya Redio na Televisheni hutolewa dakika tatu kabla ya tukio lakini kama ndio ulikuwa ukisikiliza Ndombolo ama Kijapani hakipandi kijasho kitakutoka ndugu yangu …
Usikimbie ovyo ovyo chini ya nyaya za umeme kuwa mwangalifu.
TRENI; Ukiwa ndani ya treni jisikize vyema usianguke na treni itasimama . Tulia subiri maelekezo ya wahudumu wa treni . Usiruke nje ya treni utaumia au kupoteza maisha tulia na kama hujui lugha angalia wenzako wanaelekea wapi nawe fuata.Kama una familia hebu tengeni siku moja ya kufanya mazoezi hayo …Bila shaka umefaidika na Mirindimo ya Jumamosi hii.

0 comments: