Jamaa anamuigiza St. Patrick.
Soma kidogo hapa uelewe; Saint Patrick; Huyu ni Mtakatifu mlezi wa Ireland, ndiye aliyeuingiza ukristu huko Ireland kwenye karne ya tano. Alizaliwa Uingereza na wazazi wa madhehebu ya Roma kunako mwaka 380 380AD. Alitekwa nyara akiwa na umri wa miaka 16 na kupelekwa Ireland kama mtumwa na kazi yake ilikuwa kuchunga kondoo. Wakati akiwa anachunga alipata muda mwingi wa kusoma maandiko matakatifu ya biblia ambayo alifundishwa na baba yake. Baada ya miaka sita ya kukaa utumwani alitoroka na kurudi Uingereza na kuanza safari ya kufikia ndoto yake ya kuwa Padri. Alipitia maisha ya kusisimua katika azma yake hiyo na kufanikiwa kuifanya kazi aliyodhamiria ya Upadri huko Uingereza na Ireland hadi kifo chake tarehe 17 mwaka 461. Hivyo kifo chake hukumbukwa kwa maandamano kama haya duniani kote Na watu wa Ireland huchukua fursa hiyo kujitangaza na wengine kutangaza bidhaa zao….
Ni hapa...
Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!
Posted by
BM.
on
Sunday, March 15, 2009
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

0 comments:
Post a Comment