Ni hapa...

Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!

Posted by BM. on Saturday, April 04, 2009

Mamilioni ya watu duniani kote wengi wao wakiwa nchini Uingereza wamekuwa wakifuatilia mazishi ya mtangazaji maarufu wa Reality TV ya Uingereza Jade Goody kwenye Tv zao na wengine walijitokeza na tayari msafara wa magari ukiongozwa na gari aina ya Rolls Royce limefika makaburini kupitia mitaa ya kusini mashariki mwa London.
Polisi walilazimika kusimamisha magari kupisha msafara huo hasa ulipofika katika mtaa wa Bermondsey alikokulia marehemu . Watu waliweka maua nyumbani kwake tangu jana na wengine walikuwa wakiurushia maua msafara wake huku wakinyeshewa na mvua ikionyesha kama ilikuwa sherehe Fulani kama alivyotaka marehemu Jade mwenyewe..Mama yake Jade , Jackiey Budden alionekana mtulivu wakati wote huku watu mashuhuri wakishuhudia tukio hilo akiwemo Michael Jackson.
Waandaaji wa mazishi wanasema kuwa watoto wawili wa Jade , Bobby and Freddie, wenye miaka mitano na mwingine minne inasemekana wamepelekwa nchini Austalia na baba yao Jeff Brazier kuwapunguzia simanzi na kumbukumbu ya kutisha. Jade Goody alikufa nyumbani kwake March 22 akiwa na miaka 27 bkwa ugonjwa wa kansa. Kwaheri Jade Goody.

0 comments: