Ni hapa...

Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!

Posted by BM. on Friday, April 10, 2009

Mnajimu maarufu na Mtabiri wa nyota Afrika mashariki ,Sheikh Yahaya Hussen akizungumza na waandishi wa habari jana nyumbani kwake jijini Dar es Salaam mara baada ya kuwasili toka India kwa matibabu ya ugonjwa wa moyo kulia ni mkewe Ketty (mama mufti junior). Sheikh huyo alizushiwa kufa akiwa katika matibabu India.
Hebu mtambue shekhe Yahya; Alizaliwa mwaka 1932 huko Bagamoyo kwa wazazi wakimanyema. Alipata elimu yake ya awali katika shule ya Al-Hassanain Muslim School jijini Dar-es-salaam. Baada ya hapo alikwenda visiwani Zanzibar alipojiunga na chuo kilichojulikana kama Muslim Academy kilichokuwa chini ya Sheikh Abdallah Swaleh Al-Farsy aliyekuwa Kadhi Mkuu wa Zanzibar wakati huo. Baada ya kuhitimu alielekea nchini Misri alipoendelea kusomea masuala ya dini katika chuo kikuu cha Al-Azhar kilichopo Cairo.
Alirejea nchini mnamo miaka ya mwanzoni ya 60 ambapo alianza kazi yake ya utabiri . Sheikh Yahya Hussein ndiye mtabiri wa mwanzo kueneza utabiri wa kila siku katika magazeti mbalimbali ya Afrika Mashariki enzi hizo. Jina lake lilivuma zaidi alipokuwa akitoa utabiri kupitia radio kuhusu mashindano ya mpira kati ya nchi tatu za Africa Mashariki yaliyojulikana kwa jina la Challenge Cup au Gossage Cup.

0 comments: