Ni hapa...

Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!

Posted by BM. on Friday, April 03, 2009

Mkandamizo wa mawazo yaani stress umegawanyika makundi mawili wa kawaida na ule sugu wasukuma wanauita chronic stress. Hali hii inatokea pale mwili kwa mifumo yake umeshindwa kutofautisha kuwa huu mkandamizo ni wa kisaikolojia au unahitaji msaada wa misuli. Unapojiweka katika hali ya kutojielewa bila shaka utafanya kitu usichokielewa pia . Ni kama gari lililokatika stelingi kwenye mwendo mkali. au sawa na mtu anayeendesha gari na kukwama katika foleni. Hali kama hii ikiendelea kwa muda mrefu inakupatia matatizo makubwa ya kiafya na kuvuruga mifumo yote ya mwili. Kwanza unauwezekano wa kupata shinikizo la damu, kupunguza kinga yako ya mwili dhidi ya maradhi , unaweza kupata mshituko wa moyo, kiharusi , unaweza kuharibu mifumo ya uzazi na kuharakisha ule mchakato wa kuelekea uzeeni.
Ufifiaji na michirizi katika nyuso hujitokeza mara nyingi kwa watu waliozongwa na Chronic stress.. Kisayansi sababu za mtu kufikia hali hiyo zipo nyingi lakini kubwa ni kuwa ; Baadhi ya watu wanadhani baadhi ya mambo hayako ndani ya uwezo wao kuyafahamu na kuyakabili na mara kadhaa wanajijengea hofu zaidi kuliko matumainiau kujiamini.. Watu ambao kwa hakika hawazijui tabia zao na mihemko yao na kwahiyo hawajishughulishi na kujiandalia mazingira ya kukabili hali hiyo pindi yakiwakuta. Mfano ukipata jambo linalokutia uchungu sana unafanyaje, linalokukasirisha au kukuogopesha.. Mara nyingi watu wamekuwa wakitumiamisuli mingi na kujikuta stress zao zikijiongeza siku hadi siku na kuwa wagonjwa bila kujijua.
Hali hii huwapata sana watu wanaofiwa na wapendwa wao, wanapoachika ama mahusiano kuvurugika, maisha yanapokwenda kombo , wanapokabiliwa na kesi ama kufungwa , wanapopata ajali ama ulemavu ama wanapohisi kutenda uhalifu na kuwa na wasiwasi wa kufuatiliwa na mamlaka na kadhalika.
Lakini Stress inadhibitika na hivyo kujizuia kuingia katika Chronic Stress .Swali hapa ni nini kifanyike ili kutopatwa na chronic stress ambayo inaweza Kukupunguzia siku za kuishi?…Usijaribu kuibeba dunia kichwani hutaiweza..Ungana nami katika makala ijayo ikiwa ni mwendelezo wa hii ya kwanza.

0 comments: