Kibaka mzoefu akipata kipigo kutoka kwa waumini wa Kanisa la Romani Katoliki la Mtakatifu Petro Oysterbay wakimtuhumu kuwaibia mara kwa mara vifaa vya magari yao wanapokuwa wakiwa ibada. Jumapili wakati wa misa ikiendelea vijana waliojifanya ni waokota chupa chafu za maji walijaribu tena wizi wao kwenye kanisa hilo.Kijana mmoja aliyekamatwa alipata kipigo cha kweli huku waumini wengine wakidai asamehewe na wengine wakisema haiwezekani huku wakiendelea kutoa kipigo.Baada ya kumpa kipigo waumini hao walimfikisha kibaka kwenye kituo cha polisi. Hapo ndipo linakuja suala la kusamehe kama dini zetu zinavyofundisha ...lakini kwa hili tunaliweza...sijuii
Ni hapa...
Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment