Ni hapa...

Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!

Posted by BM. on Sunday, May 03, 2009

Baba mmoja nchini Marekani ambaye alihukumiwa adhabu ya kifo baada ya kuwaua watoto wake wanne kwa kuwarusha kwenye daraja amepewa adhabu ya kuonyeshwa picha ya watoto wake aliowaua kila siku mpaka siku ya kuuliwa kwake itakapofika. Lam Luong mwenye umri wa miaka 38 mkazi wa Alabama nchini Marekani aliwaua watoto wake wanne ndani ya dakika nne kwa kuwarusha kwenye daraja mmoja mmoja.Mtoto wake mdogo kuliko wote alikuwa na umri wa miezi minne wakati mtoto wake mkubwa alikuwa na umri wa miaka miwili. Lam alitoka nyumbani kwake na watoto wake hao wanne na alipofika kwenye daraja linalounganisha jimbo la Alabama na Dauphin Island, Lam alisimamisha gari lake na kuwarusha watoto wake mmoja mmoja kwenye mto mkubwa uliokuwa unaopita mita 25 chini ya daraja hilo.Baada ya kufanya mauaji yake, Lam alipanda gari lake na kurudi nyumbani kwake kama vile hakuna kilichotokea. Bila kujua kuwa kamera zilikuwa zinammulika Kwa mujibu wa hukumu aliyosomewa Lam kutokana na tukio hilo lililotokea mwezi wa kwanza mwaka jana, pamoja na adhabu ya kifo cha kunyomwa sindano ya simu aliyopewa, mahakama iliamuru Lam aonyeshwe picha ya watoto wake aliowaua kila siku wakati anasubiria kifo chake.Mahakama ilitupilia mbali utetezi wa wakili wa Lam kwamba mteja wake alifanya tukio hilo kutokana na stress alizokuwa nazo baada ya kukosa kazi kwa miezi kadhaa. Picha za watoto wake zitabandikwa kwenye ukuta wa selo lake ili awe anaziangalia kila siku mpaka siku ya kifo chake itakapofika.

0 comments: