Jana jumatatu nilikutana na mtafiti wa masuala ya mazingira, raia wa Ujerumani katika mitaa ya Tokyo na tukakaa mgahawani kama dakika 45 hivi tukielezana yalopita. Suzan niliwahi kukutana naye Finland miaka minne iliyopita akijiandaa kwenda Tanzania. Alipojua kuwa mimi ni mtanzania wakati huo , alijitambulisha na kuniulizia juu ya mandali ya mlima Kilimanjaro aliniuliza ni kwaninii niende kuuona Mlima Kilimanjaro na sio Everest, ulio mrefu kuliko yote duniani. “Bahati”, wakati huo ilikuwa imepita miezi mitatu tu tangu niukwee mlima huo , nilikuwa na habari za kutosha kwahiyo nilijieleza bila presha.Hicho ndicho ninachotaka kukisema leo.
Pamoja na mambo mengine nilimuuliza kama alikwenda safari yake. Naam alikwenda na kukaa Tanzania wiki mbili. Akanisimulia hadithi tangu atue Dar es salaam Airport hadi kreta ya Ngorongoro na Mt. Kilimanjaro. Hadithi yake ilianza kwa changamoto. Anasema dereva aliyempeleka Hoteli ya New Africa alikofikia alimstaajabisha kidogo. Alipomuuliza juu ya maneo ya kuvutia ya Tanzania alijibu tu anafahamu Serengeti na kwamba iko km 300 kutoka Dar na sehemu nyingine ni Bagamoyo. Lakini muda mwingi alikuwa akizungumzia juu ya joto la Dar, mabomu ya Mbagala na vibaka jijini Dar akimweleza achukue hadhari.
Hotelini pia baadhi ya wafanyakazi walikuwa hawana taarifa za kutosha na hasa takwimu juu ya vivutio vyetu . Haiyumkini kuwa Suzan mwenyewe alikuwa kweli hajui …Maana alikuwa na vipeperushi kadhaa mkobani mwake lakini bila shaka alitaka kuangalia ufahamu wa watu wa kawaida wa Tanzania juu ya rasilimali walizonazo katika nchi yao. Mwisho ya yote akaniambia “Mkitaka kukuza utalii wenu wekezeni kwenye ufahamu wa watu wenu kwanza”, nikamkubalia.
Simlaumu dereva wala wafanyakazi wa New Afrika hasha. Kama nilivyopata kusema ilikuwa bahati kwa mimi kujibu lile swali vyema na pengine kwa kutumia mbinu za upaparazi.Na pengine Huko TZ Suzan angemuuliza “anayehusika” angepata maelezo ya Kutosha .Lakini tunapaswa tujiulize anayehusika si mimi na wewe , mwenzangu una habari za kutosha za nchi yetu hali ya hewa, jiografia, historia, vivutio, watu n.k kwa kiwango hicho hicho cha uelewa na elimu tuliyonayo? Unadhani kwanini dereva alijibu swali hilo hivyo. Ndipo hapo linapokuja suala la Uzalendo, lakini suala la uzalendo bila uelewa lawama…….huwezi kuvitenganisha. kazi kwelikweli! Unaonaje ukapata muhadhara wa kile kilicho chetu ili usije nawe kubabaika?
Ni hapa...
Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!
Posted by
BM.
on
Tuesday, June 16, 2009
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment