Picha ya kumbukumbu' Kutoka kushoto; Mtunzi wa kamusi mbili; Kiswahili-Kijapani na ya Kijapani-Kiswahili Mama Midori Uno kushoto, Msulwa BR, Dadaye Mama Midori na Komredi Ndesika R; a.k.a ' www.aikamangi.blogspot.com Kulia kabisa, ndani ya studio za NHK.
Moja ya kamusi alizoandika mama Midori Uno..Safii
Hebu tunekane vizuri ... ON AIR...Huyu ni Mtangazaji wa kwanza mwanamke wa kijapani katika idhaa ya Kiswahili ya Redio Japani Bi. Midori Uno. Lakini hapa mahojiano yalikuwa hatua yake ya kuandika kamusi ya Kiswahili -Kijapani na ya pili ya Kijapani(Kanji) -Kiswahili ambazo zinakurasa zaidi ya 260 kila moja . Alikuja kwa mahojiano rasmi katika studio zetu za Redio Japani- NHK idhaa ya Kiswahili.-Tokyo. Mama huyu miaka ya 70 alitumwa na serikali ya Japani nchini Tanzania -wizara ya maendeleo ya akinamama kujenga ujasiriamali na alikuwa akikaa Keko pale jijini Dar kwa wanaokujua. Hivi sasa ni mhadhiri katika vyuo vikuu mbalimbali hapa Japani. Hatua hii ya utunzi wa kamusi ambayo ina jalada lenye picha za serengeti na masai mara , na kurasa zenye ramani , nyimbo za Taifa na bendera za Kenya na Tanzania ni za kutia mooyo sana . Sio tu lugha lakini pia utalii na uchumi. Take 5 mama Midori. Unaweza kufuatilia mahojiano yetu na mama huyu kwa kufuatilia vipindi vya Ukumbi wa J2 kwa wiki tatu mfululizo kuanzia J2 hii ya 23,Aug.kwa kubofya://www.nhk.or.jp/nhkworld/swahili/top/index.html siku ya J2.
Ni hapa...
Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!
Posted by
BM.
on
Friday, August 21, 2009
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment