Mazishi ya kaburi moja kwa miili ya wanafunzi 12 yamefanyika leo jumanne katika shule ya wasichana Idodi mkoani Iringa baada ya Bweni lao kuteketea kwa moto. serikali imetangaza kuifunga shule hiyo huku ikiitaja hasara iliyopatikana , mbali na roho za watu kuwa ni shilingi milioni 105, Tukio la kusikitisha Ni wakati mgumu kwa kila mtu. Naomba tuhudhurie tukio hilo kwa njia ya picha hizi. Picha nyingine za kutisha lakini nahitaji kukupa picha halisi.
KUMRADHI, Pole sana kwa kustuka.... Naomba tugawane majonzi ya vifo hivi ; Pole sana mtazamaji. Haya ni baadhi ya Mabaki ya watoto wetu walioteketea kwa moto.;
Inauma lakini kazi ya Mungu haina nini makosa...
Mwl. mkuu akielekea kuonana na Waziri Mahiza kutoa taarifa ya tukio hilo...simanzi
Mwalimu mkuu wa shule ya sekondari ya Idodi Bw Raymond Mlasu, akiangusha kilio mbele ya Naibu waziri wa elimu na mafunzo ya ufundi Mwantum Mahiza mara baada ya kumaliza kutoa taarifa kamili kwa waziri juu ya mkasa huo. Picha zote na FrancGod kutoka Iringa..
Ni hapa...
Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!
Posted by
BM.
on
Tuesday, August 25, 2009
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment