Ni hapa...

Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!

Posted by BM. on Monday, August 24, 2009

Mmoja wa waliopiga kura Janet Metcalfe katika maombi mafupi kabla ya kuendelea na mchakato
Mashoga wakiwa wameshikana mikono wakiwa katika maandamano ya kudai haki yao kutambulika na kanisa hilo , hatimaye wamefanikiwa.
Kanisa la kiinjili la kilutheri la Marekani limepiga kura na kuruhusu wasagaji na mashoga kuwa wachungaji na viongozi wa makanisa ya kilutheri nchini humo.
Uamuzi huo wa kuwaruhusu mashoga na wasagaji kuwa wachungaji na viongozi wa makanisa ya kilutheri nchini Marekani unaonekana kuzusha mzozo na unaweza kuwagawanya wanachama wake milioni 4.6 waliopo nchini humo.
Kanisa la kiinjili la kilutheri la Marekani (ELCA) ambalo lina dayosisi zipatazo 10,000 nchini Marekani, lilipiga kura ijumaa jioni kubadilisha baadhi ya vipengele na kuwaruhusu mashoga na wasagaji kuwa wachungaji na pia kuwapa nafasi za kuwa na vyeo mbali mbali kwenye makanisa.Baada ya majadiliano makali, wawakilishi wa kanisa walipiga kura 559 za kuunga mkono kulinganisha na kura 451 zilizokuwa zikipinga wazo hilo, alisema mkurugenzi wa habari wa kanisa hilo John Brook.Kanisa la kiinjili la kilutheri la Marekani sio la kwanza nchini Marekani kutoa uamuzi huo wa kuwapa mashoga na wasagaji nafasi za uchungaji na uongozi katika makanisa. Kanisa la Episcopalian la nchini Marekani lilishawahi kutoa uamuzi kama huo.Hata hivyo uamuzi huo wa kanisa la kilutheri la Marekani haukupita kirahisi, kwani kulikuwa na upinzani mkali kutoka kwa wachungaji mbali mbali akiwemo mchungaji Richard Mahan wa dayosisi ya Maryland magharibi, Virginia.

0 comments: