Ni hapa...

Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!

Posted by BM. on Thursday, October 01, 2009


MWANAMKE mwenye asili ya Kiasia Komal Katakia[24]pichani aliyekuwa akishikiliwa pamoja na mume wake, Vinoth Praven (23) na kufikishwa mahakamani kutokana na kosa la mauaji ya mfanyabiashara mwenzao Abdulbasiti Abdallah (21) ameachiwa huru baada ya kuonekanaMshitakiwa huyo ameachiwa huru leo asubuhi mbele ya Hakimu Mkazi Kisutu Mohamed Mchengerwa Mchongero baada ya Mwendesha Mashitaka wa Serikali, Beatha Kitau, kudai kuwa haoni haja ya kuendelea kumshitaki mshitakiwa huyo.Kutokana na kauli hiyo Mahakama ilitoa amri ya kumuachia huru mshitakiwa huyo ambaye alitoka akishangilia mahakamani hapo hali iliyoonesha kuwa haamini kilichotokea dhidi yake.Alidai kuwa kwa upelelezi uliofanyika kwa kipindi kirefu umeonyesha kuwa mshitakiwa huyo ambaye ni mke wa mshitakiwa wa kwanza hakuwa na kosa hilo la mauaji.Wakati huohuo mshitakiwa Vinoth ambaye ni mume wake kesi yake imehamishiwa katika Mahakama Kuu ya Tanzania kwa ajili ya kumpangia Jaji na kuendelea kusikilizwa.Awali imedaiwa kuwa Vinoth Praven (23) na mkewe Komal Katakia ambao ni wakazi wa Kariakoo, Dar es Salaam wanakabiliwa na kesi ya mauaji dhidi ya mfanyabiashara mwenzao ambaye alichinjwa kisha maiti yake kuwekwa kwenye begi na kwenda kuitupa katika jengo la J Mall, kosa walilolifanya Februari 6, mwaka huu..Mshitakiwa Komal ameachiwa huru huku mumewe Praven akiendelea kusota kusubiri kesi yake itajwe tena katika Mahakama Kuu.

0 comments: