Soma Tarifa hii halafu jibu swali langu hapo juu;
Mamlaka ya Chakula na Dawa nchini Tanzania [TFDA] imepiga marufuku uingizwaji wa kinywaji cha Red Bull-Cola nchini humo ikieleza kuwa hatari kwa afya za binadamu kwa kuwa ina asili ya madawa ya kulevya aina ya Cocaine. Kwa mujibu wa Afisa Uhusiano wa Mamlaka hiyo, Gaudensia Simwanza mamlaka hiyo kwa sasa inaendesha msako mkali nchini kubaini watu wanaoagiza kinywaji hicho ambacho kimeshakatazwa kuingia nchini kwa sababu hizo.Alisema Mei mwaka huu walipata taarifa kwamba kinywaji hicho ni hatari na moja kwa moja mamlaka ilianza kujipanga kukidhibiti kuingia nchini. Pia alisema na kufafanua kuwa kinywaji cha Red Bull original ndio yenye madhara siyo sio Redbull cola inayoonekana mwisho wa habari hii .Hili si jambo jipya hata nchini Ujerumani katika miezi ya karibuni ilipiga marufuku kinywaji hicho baada ya Kugundua kuwa inachanganywa kidogo na Cocaine. Na kama Umeshakunywa Red Bull bila shaka umeshaionja cocaine .Pengine kwa ajili ya kujifunza Nimenukuu baadhi ya maneno kutoka makala moja “Jamiiforums.com” uwa “Kinywaji hicho kina kemikali mbaya iitwayo Glucuronolactone madhara yake ni kuwa Ni hatari kwa mtu ambaye hafanyi kazi au mazoezi mazito sana kukitumia kwani kina tabia ya kuongeza msukumo wa damu na kasi ya mapigo ya moyo kiasi kwamba mtumiaji anaweza kupatwa na ugonjwa wa moyo., Mtumiaji anaweza kupatwa na ugonjwa wa damu kuvuja ubongoni kwani RED BULL ina kemikali zinazoifanya damu iwe nyembaba ili moyo upate kusukuma damu nyingi bila kutumia nguvu nyingi. Ni hatari kuchanganya RED BULL na pombe ya aina yoyote kwani mchanganyiko wake huwa ni sumu inayoathiri musuli ila mtumiaji na kuiacha katika hali ambayo haitapona kamwe. RED BULL Ina vitamini B12 kwa wingi, vitamini ambayo hutumiwa kama dawa ya kuwazindua wagonjwa mahututi. Matumizi ya vitamini hii katika watu wazima ina athari za kuleta shinikizo la damu na humfanya mtu ajisikie kama mlevi. Unywaji wa RED BULL mara kwa mara huvuruga mfumo ya neva za fahamu nahusababisha maradhi mithili ya mfadhaiko wa akili usioponyeka. Na tafiti zimeonyesha kuwa Vijana wanaochipukia na wale wenye vijisenti vyao ndio wanaoongoza kujimaliza kila uchao na Red Bull. Wewe hujakula Cocaine kwa muhtadha huo? Acha kula hiyo kitu mwanawane!…."
Maagizo sita ya Trump yanayopaswa kuangaziwa
32 minutes ago
0 comments:
Post a Comment