Ni hapa...

Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!

Posted by BM. on Monday, October 26, 2009

Jana Jumapili kulikuwa na Maonyesho ya bidhaa za mashambani hapa Tokyo , Japani na katika pitapita yangu nikakutana na banda lina kanga , vitenge , kahawa na bidhaa nyingine kutoka Tanzania. Banda hili ni la Polepole, kamera yangu ikapata hii...
Hapo nimekutana na Mr. Tamura , Mkuu wa banda la Polepole linalouza bidhaa za Tanzania. Tumezungumza sana akinipa hadithi za Moshi na Arusha anasema "Kule safi saaana". Watu kama hawa wanaoitangaza nchi yetu wanastahili kutambuliwa na kuheshimika sana...wahusika mnasemaje!
Kahawa kutoka umatengoni...Mbingaa aisee!
Sabuni za mwarobaini zilikuwepo!

0 comments: