Ni hapa...

Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!

Posted by BM. on Friday, October 30, 2009

Ama kwa hakika , tumetoka mbali ..we acha tu.Leo nakuchukua hadi Rungwe Sekondari , shule iliyopo wilayani Rungwe , mkoani Mbeya kwa njia ya picha... nikuonyeshe shule niliyosoma, . picha kwa hisani kubwa ya Bro. Mwambegele. Hapo Kiwira mwankenja ni kilometa 15 tu kutoka Tukuyu Mjini. Km kama mbili tu kutoka hapo utaona kibao kinachokuonyesha njia ya kwenda shuleni kwetu!

Ehee hapo chepuka kulia moja kwa moja hadi Rungwe Sekondari ,chini ya Mlima Rungwee!
Mbele ya jengo hilo ndio muonekano wa Mbele , ambako kila asubuhi tulikusanyika hapo kuelewa majukumu ya siku, kukaguliwa usafi. "Asembli". Na mwanzoni mwa mwaka kuna wengi walikuwa wakiadhibiwa hapo kwa kuwabughudhi "Mugya" , jina walilokuwa wakiitwa wanafunzi wa kidato cha kwanza. Sijui leo pakoje hapo!

Ofisi za waalimu ghorofani na madarasa hapo chini...inanikumbusha mbaali.

1 comments:

Anonymous said...

Mkuu umenikumbusha mbali sana hata mimi nilisoma hapo 1980 mpaka 1983. Umenikumbusha majengo mazuli enzi hizo nikikaa Bweni la Lumumba