Ni hapa...

Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!

Posted by BM. on Friday, December 04, 2009


Peter Omari , Paparazi wa kimataifa anaendelea na jukumu maalum nchini Tanzania la kuandaa Radio Documentary inayoitwa ONE UN lengo likiwa kuonyesha mafanikio ya mashirika ya umoja wa mataifa pale yanapofanya kazi kwa pamoja (One UN) kwa kujiratibu vizuri zaidi.Tanzania ni moja ya nchi nane duniani zinazo tekeleza mpango wa pamoja wa umoja wa mataifa kwa majaribio. Nchi nyingine ni Albania, Msumbiji, Pakistan, Rwanda, Uruguay, Vietnam na visiwa vya Cape Verde. Kwa Tanzania mpango huo wa Umoja wa mataifa umeanzisha programu mbalimbali za pamoja zikikusudia pamoja na mambo mengine kuchangia kutekelezwa kwa mkakati wa kukuza uchumi na kupunguza umasikini Tanzania (MKUKUTA na MKUZA kwa Zanzibar) na pia kufanikisha kufikiwa kwa malengo ya maendeleo ya Milenia. Itl.P.P.O kwa sasa ni Meneja wa Kiss FM ya Mwanza chini ya Sahara Communication Ltd.Fuatilia kazi zake kwa njia ya Picha.
Mpanda International airport..Rukwa.
Watoto hawa walio na ulemavu wa ngozi wakiwa katika kambi ya Kabanga huko Kasulu wanalindwa na mitutu ya Bunduki kuokoa maisha yao ...Inasikitisha sana na haiingii akilini ukifikiria kuwa hiyo ndio Tanzania ya karne ya 21 Kaburi la aliyekuwa Paparazi wa kutumainiwa huko Kasulu... Kwa kifupi Deogratius Kiduduye alifariki dunia Mwezi May mwaka huu kwa ugonjwa wa kisukari kwa mujibu wa matangazo yaliyotolewa na Radio Free Afrika,Mwanza ambako alikuwa miongoni mwa watangazaji wa kwanza walioanzisha redio hiyo hapaTanzania .Mpaka mauti yanamkuta Kiduduye alikuwa ni mtangazaji katika kituo cha Radio Uhuru cha jijini Dar es salaam. Ana kila sababu ya kukumbukwa.
Enzi ya uhai wake Marehemu Kiduduye picha ya Juu (KUSHOTO) akiwa Lusaka Zambia. Picha kwa hisani ya Mtangazaji Blog. Peter Omari alifika kwa mama yake Kiduduye kuhani. Picha ya Kumbukumbu.

Ukiona kibao umefika! Mdau mara baada ya kumalizika kwa mkutano wa wanavijiji wanaoishi jirani na kambi ya wakimbizi ya Viyowesi -Kasulu
Katika Majukumu;Afisa Mipango wa wilaya ya Kasulu Bw. Bwire Mjuberi akiongea na Int.PP.O

0 comments: