Ni hapa...

Umefika mahali unapopahitaji ...karibu!

Posted by BM. on Thursday, December 31, 2009

Mzee Rashidi Mfaume Kawawa katikati akisalimiana na Raisi Jakaya Kikwete amefariki dunia asubuhi katika hospitali ya Muhimbili katika chumba cha wagonjwa mahututi. Kulia ni mke wa Marehemu kawawa. Kwa kifupi; Mzee Rashidi Mfaume Kawawa alizaliwa tarehe 27 February, 1926 katika kijiji cha Matepwende, Wilaya ya Songea, Mkoani Ruvuma, Tanzania. Alianza elimu ya msingi huko Liwale, Lindi mnamo 1941 - 1942 na kuendelea na masomo ya sekondari katika shule ya skondari Dar es salaam,. Huyu ni mwanasiasa mwenye historia ndefu lakini itoshe kusema tu kwamba kuanzia tarehe 22 Januari, 1962 hadi tarehe 13 Februari, 1977 alikuwa Waziri Mkuu wa Tanzania. Alifuatwa na Edward Sokoine. Baadaye alikuwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi. Raisi Jakaya Kikwete akilihutubia taifa mchana wa leo wakati akitangaza kifo cha Mzee rashidi Mfaume Kawawa . Taifa litakuwa kwenye maombolezo kwa siku saba ambapo bendera zitapepea nusu mlingoni. Mungu ailaze roho ya Mzee Kawawa peponi Amin. Nyumbani kwa Mzee Kawawa Madale, Dar es salaam.

0 comments: