Muda mfupi uliopita usiku huu wa Jumamosi hafla imekwisha katika Chuo Kikuu cha Soka hapa Japani, ambapokulifanyika mashindano ya 19 ya hotuba kwa lugha ya Kiswahili ya kuwania kombe la mwasisi wa Chuo kikuu cha Soka Bw. Daisaku Ikeda. Pitia Picha hicho ili upate picha ya kile kilichotokea leo....Hapo ni jumba moja ya Chuo hicho ambacho huifadhi nyaraka na medali mbali ambazo chuo hicho imepata katika hafla mbalimbali...
Timu nzima ya waalikwa kwenye mashindano hayo. Kushoto mwongozaji wetu Afisa wa Ubalozi wa Tanzania Mr. Francis Musongo , Bm , Mwakilishi wa Balozi wa DRC hapa JP Mulumba Tshindimba Mr. Mwenda na Bi Grace wa Ubalozi wa Tz hapa JPna mwongozi wetu mwingine. Pozi la chapchap!
Nami nilipata kuzungumza kama mmoja wa majaji.. Burudani nayo ilikuwepo...
Da Mariamu akiwa na mshindi... Hawa ndio Ma Mc wa shughuli yaleo hapa Soka university..wamefanya kazi nzuri sana.
Picha ya pamoja; Grace, mshindi wa kwanza Bi.Masako Kitaura,Afisa mwandamizi wa Ubalozi wa Tanzania Japani Fancis Mussongo Da Mariam, Bw. Mwombeki , Kiongozi wetu mwandamizi wa Jumuia ya watanzania wanaoishi Japani ,BM.
Mmoja wa Viongozi waandamizi wa TANZANITE -JP Mr. Mwombeki (Kulia)alikuwepo.
Watanzania walifika kutoa support ya kukuzwa kwa Kiswahili....
Maagizo ya rais ni nini?
1 hour ago
0 comments:
Post a Comment